Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Cecil David Mwambe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ndanda
Primary Question
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza kujenga Madaraja ya Chikundi katika Wilaya ya Masasi?
Supplementary Question 1
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, ni kweli kazi hizo zinaendelea. Niliweke sawasawa, ni Kata ya Chikundi, siyo kama vile ambavyo Mheshimiwa Naibu Waziri ameitamka. Tunalo pia Daraja la Liputu – Ng’uni, tunalo pia Daraja la Nango’o – Ng’uni. Pia tushukuru kwa sababu ya Daraja la Litama Mbaju. Nataka kufahamu ni lini Daraja la Liputu ambalo wakazi wa Ndanda wamekuwa wanalitumia kuvuka kwa ajili ya kwenda kwenye masuala ya kilimo, upande wa pili wa upande wa Ruangwa kupitia Kivuko cha Nguni na Kivuko cha Nangoo. Je, ni lini madaraja haya yatajengwa?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Cecil Mwambe kwa maswali yake yanayolenga kuwasemea wananchi wake kupata miundombinu bora kabisa ya barabara hizi za wilaya.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia TARURA kwenye mpango wa kukabiliana na dharura imetenga bilioni 2.5 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Ng’uni. Tayari usanifu umeshafanyika na taratibu za manunuzi zinaendelea na zinatarajia kwisha; mwezi wa tatu zitakuwa zimekamilika kwa ajili ya ujenzi kuanza.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika ujenzi au uboreshaji wa Daraja la Ng’uni, daraja hili litakuwa ni lile daraja la chuma ambalo kwa jina la kitaalam wanasema ni mabey bridge. Litakuwa lina urefu wa mita 30 na litakuwa na madaraja mawili saidizi. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inatambua umuhimu mkubwa sana wa miundombinu hii ya barabara na madaraja haya kwa sababu wananchi wanajishughulisha na shughuli za kilimo pia wanatumia barabara hizi kufikia huduma muhimu kabisa za kijamii. Nimhakikishie kwamba Serikali itaendelea kuhudumia barabara hizi za wilaya katika jimbo lake.
Name
Minza Simon Mjika
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza kujenga Madaraja ya Chikundi katika Wilaya ya Masasi?
Supplementary Question 2
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kijiji cha Buriashi na Mwamagingo hakuna daraja kabisa na daraja lile ni muhimu kwa sababu kuna wanafunzi wanaotoka Mwamagingo kwenda Buriashi Sekondari hakuna Daraja. Je, ni lini Serikali itajenga daraja ili kurahisisha mawasiliano kwa wakazi wa Wilaya ya Meatu?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nianze kumpongeza Mheshimiwa Minza kwa swali lake lenye lengo la kuhakikisha wananchi wa Meatu wanapata miundombinu ya barabara.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inatambua umuhimu mkubwa wa barabara hizi za wilaya kwa sababu ya barabara hizi ndio zinazosaidia wananchi katika shughuli zao za uzalishaji mali na ndizo hizi zinazowawezesha wananchi kufikia huduma muhimu kabisa za kijamii.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie kwamba Serikali kwa kutambua umuhimu wa barabara hizi na ndiyo maana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uongozi wake wa miaka minne amepandisha bajeti ya kuhudumia barabara hizi kutoka bajeti ya bilioni 275 kwa mwaka hadi sasa kila mwaka bajeti ni milioni 710. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea kufika maeneo mbalimbali nchini ili kuunganisha mawasiliano katika maeneo yale ambayo mawasiliano yamekatika ikiwemo maeneo haya yenye vivuko na madaraja. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itafika Meatu na itakuja kujenga daraja hilo.
Name
Selemani Moshi Kakoso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpanda Vijijini
Primary Question
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza kujenga Madaraja ya Chikundi katika Wilaya ya Masasi?
Supplementary Question 3
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, Barabara ya Kapanga – Bujombe ipo hatarini kutokupitika baada ya mkandarasi kushindwa kujenga madaraja. Je, ni lini Serikali itamsimamia mkandarasi huyu ili aweze kukamilisha ujenzi wa madaraja haya?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimpongeze Mheshimiwa Selemani Kakoso kwa swali lake zuri lenye maslahi mapana kwa ajili ya wananchi wake, wapiga kura wake.
Ninaomba nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kumwagiza Meneja wa TARURA wa mkoa kufika na kufuatilia changamoto inayokabili ujenzi wa daraja hili ili tuweze kusimamia kwa ufanisi na daraja hili liweze kukamilika kwa mujibu wa mkataba.
Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri wa Nchi amekuwa akitoa maagizo mara kwa mara na akisisitiza, kwamba wakandarasi wanapopatiwa kazi hizi za ujenzi wa barabara wazingatie mkataba na wafanye kazi kwa ufanisi kwa viwango na wakati. Kwa hiyo, Meneja wa TARURA wa mkoa aweze kusimamia maelekezo haya ambayo yametolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved