Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 12 Energy and Minerals Wizara ya Nishat 202 2025-02-12

Name

Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha Magari ya Serikali yanakuwa na mfumo wa nishati ya gesi?

Name

Doto Mashaka Biteko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukombe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuwezesha Serikali kuanza kutumia magari yanayotumia gesi Serikali katika imejikita kuweka miundombinu ya kuwezesha matumizi ya CNG kwenye magari ya Serikali kwa urahisi. Serikali kupitia GPSA (The Government Procurement Services Agency) imekwishaanza taratibu za kuweka miundombinu kwa ajili ya magari ya Serikali yatakayotumia gesi ikiwemo kufanya tathmini za athari za kijamii na mazingira pamoja na uandaaji wa michoro ya kina ya kihandisi na usimamizi wa ujenzi. Taratibu hizi ni kuweka miundombinu rafiki kwa magari ya Serikali kuanza kutumia gesi.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, ili kuboresha upatikanaji wa CNG kwa mikoa iliyo katika barabara kuu kuelekea Dodoma, Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) ipo kwenye hatua za manunuzi za mradi wa kuagiza na kusimika vituo vya CNG vinavyohamishika; ambapo kwa kuanzia vituo vitatu vitasimikwa Dar es Salaam, kimoja kitasimikwa Morogoro na viwili vitasimikwa Dodoma.