Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 12 Energy and Minerals Wizara ya Nishat 203 2025-02-12

Name

Kenneth Ernest Nollo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bahi

Primary Question

MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani kuhuisha zaidi kasi ya usambazaji wa umeme nchini?

Name

Doto Mashaka Biteko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukombe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kuongeza kasi ya usambazaji umeme nchini kupitia miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya kupeleka umeme vijijini ambapo imeweza kufikisha umeme katika vijiji vyote 12,318 Tanzania Bara na vitongoji 33,657 kati ya vitongoji 64,359, sawa na 52.3%.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na kasi hiyo ya usambazaji wa umeme nchini idadi ya wateja imeongezeka kutoka wateja 4,689,024 waliokuwepo mwezi Januari, 2024 hadi kufikia wateja 5,276,679 mwezi Desemba, 2024, sawa na ongezeko la 12.5%. Aidha, kupitia Mpango Mahususi wa Taifa wa Nishati, Serikali imelenga kuongeza kasi ya usambazaji wa umeme nchini kutoka 78.4% hadi 100% ifikapo mwaka 2030.