Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Kenneth Ernest Nollo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bahi
Primary Question
MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani kuhuisha zaidi kasi ya usambazaji wa umeme nchini?
Supplementary Question 1
MHE. KENNETH E. NOLLO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninaishukuru Serikali kwa majibu mazuri. Vilevile, ninaishukuru Serikali kwa jitihada za kufikisha umeme katika maeneo ya wananchi. Swali langu la kwanza; pamoja na kwamba katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 nimepata vitongoji 15, lakini Bahi ina vitongoji 520. Je, nini ahadi ya Serikali katika kuongeza kasi ya kuweka umeme zaidi katika vitongoji vingine? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Kitongoji cha Mgondo kilichopo katika Kijiji cha Kongogo katika Kata ya Babayu ni kitongoji chenye sura ya kijiji. Vilevile, Kitongoji cha Majengo kilichopo Kata ya Mpalanga Kijiji cha Chidilo nacho kina sura ya kuwa kijiji. Vitongoji hivi vikubwa bado havijapata umeme. Ni nini mkakati wa Serikali katika kufanikisha vitongoji hivi viwili vya Mgondo na Majengo viweze kupata umeme? (Makofi)
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kwa pamoja kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kupeleka umeme katika jimbo la Mheshimiwa Mbunge. Katika mwaka huu wa fedha, Serikali imejipanga kuhakikisha inakuja na mpango mwingine wa kupeleka umeme kwenye vitongoji. Mpango huu utatangazwa hivi karibuni na tunatarajia katika Jimbo la Mheshimiwa Mbunge vitongoji visivyopungua 70 vitapatiwa umeme. Katika maeneo yale ambayo ameyataja basi yatazingatiwa katika huu mradi mpya ambao unakusudiwa kutangazwa hivi karibuni. (Makofi)
Name
Dr. Christine Gabriel Ishengoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani kuhuisha zaidi kasi ya usambazaji wa umeme nchini?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali. Je, ni lini Serikali itapeleka umeme kwenye Kijiji cha Madudumizi B ambacho hakina umeme kwenye Kata ya Zombo, Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa? Ahsante. (Makofi)
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema, tayari tumekamilisha kupeleka umeme kwenye vijiji, kazi iliyopo sasa ni kupeleka kwenye vitongoji. Kwa sasa, kila jimbo linapelekewa vitongoji 15, lakini hivi karibuni tutatangaza mpango mwingine ambao unatarajiwa kupeleka umeme kwenye vitongoji vingine zaidi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved