Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 12 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 204 2025-02-12

Name

Abdallah Dadi Chikota

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyamba

Primary Question

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:-

Je, lini awamu ya pili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini utaanza?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa awamu ya pili wa Hospitali ya Kanda ya Kusini, Mtwara unaojumuisha ujenzi wa jengo la mama na mtoto, ujenzi wa nyumba za watumishi, ujenzi wa kichomea taka, ujenzi wa jengo la kufulia na tayari usanifu wa michoro umeshakamilika na taratibu za kumpata mkandarasi zimekwishaanza na zabuni imeshatangazwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kulithibitishia Bunge lako kuwa mpaka kufikia mwezi Aprili 2025, awamu ya pili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini utakuwa umeanza. Ninaomba kuwasilisha.