Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 12 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 205 2025-02-12

Name

Aida Joseph Khenani

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza:-

Je, Serikali haioni haja kwa sasa kutoa huduma na dawa kwa wagonjwa wa kifafa bure?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikitoa matibabu kwa wagonjwa wa kifafa katika ngazi zote za huduma nchini. Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 takribani wagonjwa 199,324 walipatiwa huduma za matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya hapa nchini. Kwa mujibu wa mwongozo wa matibabu yaani Standard Treatment Guidelines (STG) kuna takribani aina nane za dawa za msingi za matibabu ya kifafa ambazo hutolewa kuanzia ngazi ya msingi ambapo dawa hutolewa kulingana na hali ya ugonjwa. Huduma za matibabu ya kifafa hutolewa kwa mujibu wa Sera ya Afya ya mwaka 2007.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kulithibitishia Bunge lako Tukufu kuwa Serikali itaendelea kutoa huduma za dawa kwa wagonjwa wa kifafa na kuhakikisha huduma hizo zinapatikana katika ngazi zote za vituo vya kutolea huduma. Ninaomba kuwasilisha.