Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Aida Joseph Khenani
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Nkasi Kaskazini
Primary Question
MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza:- Je, Serikali haioni haja kwa sasa kutoa huduma na dawa kwa wagonjwa wa kifafa bure?
Supplementary Question 1
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Naibu Spika, nimesikia majibu ya Serikali, lakini nina maswali madogo mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; mwaka 2023 Shirika la Afya Duniani lilitoa tathmini yake kwamba wagonjwa milioni 50 walibainika kuwa na kifafa, lakini kila mwaka walibainika wagonjwa milioni tano.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika nchi zenye kipato cha kati na cha chini tukiwemo Tanzania, kati ya watu 100,000, watu 139 wamebainika wana kifafa. Ni ipi programu maalum ya Taifa ya kuweza kutoa elimu kulingana na ukubwa wa tatizo hili? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; amezungumzia matibabu wanayoyatoa. Changamoto zinazopelekea idadi kubwa ya wagonjwa wa kifafa ni pamoja na ajali, watoto wanapozaliwa, wanawake wanapojifungua na sababu nyingine nyingi. Wizara haioni kwamba ni muda muafaka wa kuanza kutoa matibabu haya mapema kwa sababu kifafa kinatibika? (Makofi)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninampongeza dada yangu, Mheshimiwa Khenani, ameuliza swali la msingi sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli ni mojawapo ya magonjwa ambayo wakati mwingi watu wengi wamekuwa hawajui kwamba yapo. Watu wengi wapo mtaani na hawapelekwi hospitalini kwa hiyo, ni sehemu moja kubwa muhimu ya hamasa kuhusu ugonjwa huo na watu waweze kutuletea watu hospitalini.
Mheshimiwa Naibu Spika, siku ya Jumatatu sikuwepo hapa Bungeni, ilikuwa ni siku maalum kwa ajili ya wagonjwa wa kifafa. Kwa hiyo, ninamwambia Mheshimiwa katika maswali yake haya mawili; moja, kwamba wako wengi tunawatambuaje mapema?
Mheshimiwa Naibu Spika, moja, tumeanza kampeni kwa kutumia madaktari wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, moja ya ajenda yetu ya kudumu kwa madaktari wale ni pamoja na kutambua wagonjwa wa kifafa na kuwaleta pale na kuanza kuwatibu on site ili na wataalam walioko pale wajifunze hizo knowledge walizonazo specialists wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pia ameshatoa maelekezo kwamba kuanzia sasa haya magonjwa mengi, siyo kifafa tu, mtoto aanze kufuatiliwa toka mimba inavyotunga, anapozaliwa a-screen-iwe magonjwa yote mpaka upofu na mambo mengine kuhakikisha kila ugonjwa unajulikana mapema, yale yenye tiba tuweze kutibu mapema. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved