Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 12 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 206 | 2025-02-12 |
Name
Kilumbe Shabani Ng'enda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kigoma Mjini
Primary Question
MHE. JOSEPH M. MKUNDI K.n.y. MHE. KILUMBE S. NG’ENDA aliuliza:-
Je, lini wananchi wanaozunguka Ziwa Tanganyika watapata elimu na nyenzo za kuanzisha ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba?
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wameendelea kujenga uwezo wa kufuga samaki kwa njia ya vizimba kwa wananchi wanaozunguka Ziwa Tanganyika ambapo, jumla ya wananchi 302 wamepatiwa mafunzo kuhusu mbinu bora za ufugaji samaki kwa njia ya vizimba. Vilevile, Wizara kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) inaendelea na zoezi la ugawaji wa nyenzo za ufugaji wa samaki ambapo jumla ya vizimba 29, vifaranga na chakula vyenye thamani ya shilingi milioni 602 vimetolewa kwa mikopo ya masharti nafuu isiyokuwa na riba kwa wanufaika katika Mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi.
Mheshimiwa Naibu Spika, hadi sasa, jumla ya vizimba 16 vimesanikishwa katika eneo la Katabe, Mkoani Kigoma na zoezi la upandikizaji wa vifaranga linaendelea. Aidha, Wizara itaendelea na zoezi la ugawaji wa pembejeo kwa wanufaika wengine kulingana na upatikanaji wa fedha. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved