Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph Michael Mkundi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Primary Question

MHE. JOSEPH M. MKUNDI K.n.y. MHE. KILUMBE S. NG’ENDA aliuliza:- Je, lini wananchi wanaozunguka Ziwa Tanganyika watapata elimu na nyenzo za kuanzisha ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu ya Serikali. Kwa kuwa, elimu hii ni muhimu sana si kwa Ziwa Tanganyika tu, lakini kwa maeneo yote ya ziwa hasa Ziwa Victoria ambako sehemu kubwa ya wananchi wanategemea uvuvi. Je, ni nini mkakati wa Serikali kutoa elimu hii kwenye eneo lote la Ziwa Victoria hasa maeneo ya Ukerewe ambako shughuli kubwa ya kiuchumi ni uvuvi? (Makofi)

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika jibu la msingi, tumeanza kutoa elimu kwenye Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria, lakini pia Ziwa Nyasa na kwenyewe tayari tumeshatuma wataalam kwenda kuainisha maeneo ambayo tunaweza kuweka vizimba.

Mheshimiwa Naibu Spika, namwondoa wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba, maeneo yote yanayozunguka Ziwa Victoria, tayari tuna wataalam wetu kupitia Maafisa Ugani, Maafisa Uvuvi waliokuwa kwenye maeneo hayo, wanaendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuanzisha vizimba katika maeneo yao yanayowazunguka. Kwa hiyo, hilo tayari tumeanza katika maeneo mbalimbali ya maziwa yote makubwa yaliyoko ndani ya nchi yetu, lakini pia katika mabwawa ambayo yanazunguka maeneo ya vijiji vyetu. Ahsante.