Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 12 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 207 2025-02-12

Name

Jafari Chege Wambura

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rorya

Primary Question

MHE. JAFARI W. CHEGE aliuliza:-

Je, lini Serikali itahimiza kuwa na zao la kimkakati Mkoa wa Mara?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA MADINI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kulingana na ikolojia ya Mkoa wa Mara, mazao ya kimkakati yanayohimizwa ni pamoja na pamba, kahawa, tumbaku, alizeti, muhogo na mazao ya jamii ya mikunde ikiwemo dengu na choroko. Wakulima wanashauriwa kufuata kanuni bora za kilimo ili kuhakikisha wanazalisha mazao hayo kwa tija kwa lengo la kuongeza usalama wa chakula na kipato kwenye kaya.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha mazao hayo yanapewa kipaumbele na kuzalishwa kwa tija kwa kuimarisha huduma za ugani, kuhamasisha wawekezaji katika miundombinu ya umwagiliaji, uhifadhi, uchakataji na kuimarisha masoko ya mazao hayo.