Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 12 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 208 2025-02-12

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza:-

Je, lini ujenzi wa Common Use Facility utaanza kwa kuwa ilishawekwa kwenye bajeti?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA MADINI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Wizara ilitenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Kuhifadhi Mazao ya Bustani (Common Use Facility) kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Hai. Hata hivyo, baada ya kufanyika tathimini, ilibainika kuwa hitaji kubwa la halmashauri hiyo ni soko kwa ajili ya kuuzia mazao yao. Hivyo, Halmashauri ya Wilaya ya Hai walibadili na kuanza ujenzi wa soko unaoendelea katika eneo la Mula katika halmashauri hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa Wizara inaendelea na ujenzi wa vituo viwili vya kuhifadhi mazao ya bustani katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Mkoani Mbeya ambazo zilitoa maeneo yenye umiliki wa hati pacha. Aidha, Wizara itaendelea na ujenzi wa vituo hivyo, kwenye maeneo mengine yenye uhitaji na yatakayokidhi vigezo vya kuwa na vituo vya kuhifadhi mazao ya bustani.