Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Common Use Facility utaanza kwa kuwa ilishawekwa kwenye bajeti?

Supplementary Question 1

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; Soko hili la Mula lilitangazwa na mkandarasi akapatikana, lakini hivi karibuni tumeambiwa kuna makosa ya kitaalam yalifanyika ambayo yanazuia soko hili lisianze kutangazwa, nami waliniambia siku ya Jumamosi tunaenda kukabidhi mkandarasi aanze ujenzi. Je, ni lini sasa mkandarasi huyo ataanza kujenga Soko letu la Mula?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Chama cha Mroso Sangi kwa maana ya Shamba lile la Kibo na Kikafu, tuliingia mkataba na Kampuni ya MackJaro kwamba ajenge kiwanda cha parachichi, mpaka sasa hivi hajaanza ujenzi wa kiwanda hiki wakati kwenye workplan tulikubaliana mwaka 2024 aanze ujenzi. Je, ni lini sasa kiwanda hiki cha parachichi kitaanza kujengwa kwenye Shamba la Kibo Kikafu?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

WAZIRI WA MADINI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza, ni kweli ilitokea changamoto katika Mfumo wa Nest, ilivyopandishwa ile zabuni, ilionekana kuna details nyingi sana zinakosekana. Hivyo natumia fursa hii, kumuarifu Katibu Mkuu na kumtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo chini ya Idara ya Masoko, kuhakikisha kwamba wanapitia na ku-address changamoto zilizojitokeza ili zabuni hii itangazwe kwa haraka, wananchi wa Hai waanze kunufaika na Soko hilo la Mula kadri itakavyowezekana.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili kuhusu ujenzi wa kiwanda cha parachichi katika eneo lile la Mroso Sangi ambapo yaliingiwa makubaliano na workplan iko pale, ni kweli ilipaswa itekelezwe na haijatekelezwa mpaka hivi sasa. Hivyo natumia fursa hii kumwelekeza Mrajisi wa Tume ya Ushirika kuhakikisha anasimamia utekelezaji wa workplan hii ili ujenzi wa kiwanda hiki uanze mara moja, wananchi wa Hai wanufaike na mradi huu mkubwa wa parachichi.