Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 12 | Finance | Wizara ya Fedha | 209 | 2025-02-12 |
Name
Ussi Salum Pondeza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chumbuni
Primary Question
MHE. MIRAJI J. MTATURU K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA aliuliza:-
Je, Serikali imechukua hatua gani za kuhakikisha huduma za kubadilisha fedha zinapatikana karibu na Hoteli za kitalii Zanzibar?
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, hatua zilizochukuliwa na Serikali kuwezesha upatikanaji wa huduma za kubadilisha fedha za kigeni kwa urahisi nchini ikiwemo Zanzibar, ni kurekebisha Kanuni za Maduka ya Kubadilisha Fedha za Kigeni za Mwaka 2019 na kutoa kanuni mpya za mwaka 2023 na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali Na. 42 la Oktoba, 2023 ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kubadilisha fedha za kigeni nchini. Katika utoaji wa leseni, kanuni zimeweka madaraja matatu ya maduka (Daraja A, B na C) na kupunguza mtaji unaohitajika katika kuanzisha maduka hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, mabadiliko hayo yametoa fursa kwa hoteli zenye hadhi ya nyota tatu au zaidi kuomba leseni za kufanya biashara ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni kupitia dirisha la daraja C. Kufuatia marekebisho haya, idadi ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni Zanzibar imeongezeka kutoka maduka 4 yenye matawi 11 hadi kufikia maduka 15 yenye matawi 35. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved