Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Miraji Jumanne Mtaturu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Mashariki
Primary Question
MHE. MIRAJI J. MTATURU K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA aliuliza:- Je, Serikali imechukua hatua gani za kuhakikisha huduma za kubadilisha fedha zinapatikana karibu na Hoteli za kitalii Zanzibar?
Supplementary Question 1
MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kanuni mpya zimesaidia kwa kiasi gani uendeshwaji wa maduka ya kubadilishia fedha za kigeni?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; mwaka 2017/2018, kulikuwa na utaratibu wa kuzuia leseni au kusitisha leseni za hawa wafanyabiashara wanaofanya biashara hii ya fedha za kigeni katika Mikoa ya Arusha na Dar es Salaam. Je, maduka yalikuwa mangapi na sasa hali ikoje ili shughuli ziendelee kama kawaida kwa wananchi hao? Ahsante sana.
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mtaturu kama ifuatavyo, lakini kabla ya kujibu maswali hayo, naomba kumpongeza sana Mheshimiwa Mtaturu kwa ufuatiliaji mkubwa wa suala hili.
Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria hii imesaidia kwa kiasi kikubwa sana na ndiyo maana kwenye jibu langu la msingi nikasema, kwamba hata ongezeko la maduka ya ubadilishaji wa fedha za kigeni yameongezeka kutoka nne hadi kufikia 15. Hii ni kwa sababu pia ya punguzo lililopo kwenye mtaji ambao umegawiwa katika madaraja matatu.
Mheshimiwa Naibu Spika, Daraja A gharama yake ya mtaji ni shilingi 1,000,000,000, Daraja B ni shilingi 500,000,000 na Daraja C shilingi 200,000,000. Kwa hiyo, imeongeza idadi ya huduma hii ya maduka ya kubadilisha fedha.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, ni kweli mwaka alioutaja ilitokea kufutwa leseni kwa baadhi ya maduka na alitaka kujua idadi. Idadi ya maduka hayo yalikuwa ni 65 lakini kwa bahati nzuri maduka 61 tayari yamesharejeshewa gharama zao na yamepewa leseni huduma inaendelea. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved