Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 12 Works and Transport Wizara ya Uchukuzi 210 2025-02-12

Name

Stella Ikupa Alex

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. STELLA I. ALEX aliuliza:-

Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha miundombinu na mazingira ya usafiri kwa watu wenye ulemavu inakuwa rafiki katika treni ya SGR?

Name

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkoani

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI K.n.y. WAZIRI WA UCHUKUZI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa miundombinu ya reli pamoja na majengo umezingatia uwepo wa miundombinu wezeshi kwa watu wenye mahitaji maalumu ikiwa ni pamoja na uwekaji wa alama maalum zinazowasaidia kuwaongoza ndani ya majengo pamoja na huduma ya maliwato kwa kuweka vyoo maalum. Vilevile, katika mabehewa tumezingatia uwepo wa sehemu maalum kwa ajili ya kuwawezesha watu wenye mahitaji maalum kuweka viti vyao (wheel chair) pamoja na uwepo wa nukta nundu kuwasaidia kuona.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Shirika la Reli limenunua na litaendelea kununua na kuweka viti maalum (wheel chairs) katika majengo ya stesheni kwa lengo la watu wenye mahitaji maalum kutopata changamoto za utumiaji wa huduma za treni. Ahsante.