Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Stella Ikupa Alex

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. STELLA I. ALEX aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha miundombinu na mazingira ya usafiri kwa watu wenye ulemavu inakuwa rafiki katika treni ya SGR?

Supplementary Question 1

MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kuipongeza na kuishukuru sana Serikali, pamoja na kwamba SGR ina muda mfupi katika utendaji wake, lakini mambo mengi yamekwishafanyika kwa kundi hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; Serikali inaonaje sasa ikachukua ule utaratibu ambao umekuwa ukitumika na viwanja vya ndege kote duniani, kwa kuwa na watumishi maalum wa kulihudumia kundi hili pale wanapofika kwenye vituo, mpaka kuwawezesha kuingia kwenye treni. Tofauti na ilivyo sasa hivi, wamekuwa wakipata shida wanapofika kwa sababu kila mtu anaona siyo jukumu lake kuhudumia mtu kama huyu yaani ni mpaka mtu ajitolee.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; ninaishukuru Serikali kuna ngazi mserereko kwenye SGR lakini ngazi mserereko hizi ni too steep. Ninaomba Serikali iweze kuzibadilisha na ziwekwe ngazi mserereko ambazo zinakuwa zina gentle slope. Ahsante.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naanza kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa sababu mambo mengi yameendelea kuboreshwa kutokana na maombi yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge pamoja na Waheshimiwa Wabunge kwamba maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kuhakikisha kwamba safari za treni na hasa SGR zinakuwa bora na rafiki lakini pia kuwa na viwango vya kimataifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, tutaendelea kuboresha kadri tutakavyokuwa tunapata maoni. Kwa maswali yake yote mawili, moja la kuwa na wasaidizi, lakini pia kuwa na ngazi mserereko rafiki (ramp), ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali tumelichukua na tutahakikisha kwamba katika kurekebisha hizo ngazi mserereko, tutahitaji pia tuweze kuwashirikisha wanufaika ikiwa ni pamoja na mambo mengine kuhakikisha kwamba usafiri wa SGR unakuwa ni rafiki. Ahsante.