Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 12 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 211 2025-02-12

Name

Selemani Jumanne Zedi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukene

Primary Question

MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza:-

Je, kuna mpango gani wa kutoa mafunzo ya utaalam, mitaji, kuwaunganisha na masoko wajasiriamali wanaoongeza thamani ya mazao?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo Tanzania (SIDO) inaendelea na utekelezaji wa mpango wake wa kuwawezesha wajasiriamali katika shughuli zao ikiwa ni pamoja na uongezaji thamani mazao.

Mheshimiwa Naibu Spika, utekelezaji huo hufanywa kwa kutoa mafunzo, ushauri, uwezeshaji upatikanaji wa teknolojia za usindikaji wa mazao ya kilimo na uchakataji wa bidhaa mbalimbali, kuwawezesha Wajasiriamali kupata mitaji ambapo SIDO imekuwa ikitoa mikopo midogo pamoja na kuwaunganisha wajasiriamali wenye mahitaji ya mikopo mikubwa na Taasisi za kifedha ambazo Shirika limeingia nazo makubaliano.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuwaunganisha pia wajasiriamali kushiriki katika maonesho yanayoandaliwa na wadau mbalimbali kitaifa na kimataifa kwa lengo la kutangaza bidhaa na kupata soko la bidhaa zao. Ninakushukuru.