Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 12 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 212 2025-02-12

Name

Janeth Elias Mahawanga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza:-

Je, lini TBS itaweka utaratibu wa kutoa elimu kwa Wajasiriamali wadogo wanaojihusisha na biashara ya kusindika vyakula?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS), imekuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo kwa Wajasiriamali wadogo na wa kati wanaojihusisha na biashara ya kusindika bidhaa mbalimbali ikiwemo bidhaa za vyakula. Mafunzo hayo hutolewa kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa Shirika na Mpango Kazi wa Mafunzo kwa Wajasiriamali unaoandaliwa kila mwaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika utekelezaji wa mpango huo, mafunzo hayo ambayo yamekuwa yakitolewa kwa kushirikiana na SIDO na utaratibu huo umesaidia, si tu kusindika vyakula, bali na kupata teknolojia sahihi zinazosaidia kuzalisha bidhaa zenye viwango, lakini pia kupata mikopo, majengo na elimu ya biashara na masoko. Ninakushukuru sana.