Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 12 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 214 2025-02-12

Name

Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SHALLY J. RAYMOND aliuliza:-

Je, vituo vingapi vya umahiri vya sayansi na teknolojia na Akili Mnemba katika Taasisi za Elimu ya Juu vimeanzishwa?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeanzisha jumla ya vituo vya umahiri 13 kati ya vituo 13, sawa na 100% ya lengo la miaka mitano katika Taasisi za Elimu ya Juu. Lengo la kuanzishwa kwa vituo hivyo ni kuimarisha uwezo katika utoaji wa elimu ya juu na utafiti katika maeneo ya afya na baiolojia ya molekuli; TEHAMA; kilimo na mifugo; maji na nishati jadidifu. Aidha, Serikali itaendelea kuanzisha vituo vipya vya umahiri kulingana na mahitaji, hususan katika kuimarisha mchango wa utafiti na ubunifu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Ninakushukuru sana.