Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Shally Josepha Raymond
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND aliuliza:- Je, vituo vingapi vya umahiri vya sayansi na teknolojia na Akili Mnemba katika Taasisi za Elimu ya Juu vimeanzishwa?
Supplementary Question 1
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali langu la kwanza la nyongeza; ningependa kufahamu kuhusu TEHAMA katika hivyo vituo 13, je, matumizi ya Akili Mnemba (Artificial Intelligence) yako kwa kiwango gani?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; taasisi binafsi za elimu ya juu zinawezeshwa vipi na Serikali kwa kuanzisha vituo vya umahiri vya sayansi na teknolojia? (Makofi)
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Shally Raymond, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, masuala ya Akili Mnemba (Akili Unde/Artificial Intelligence) lengo kuu la hii AI inatumika kama kiwezeshi. Sasa ninaomba tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako Tukufu lengo la matumizi ya akili hizi ni kuimarisha ubora pamoja na teknolojia katika bidhaa mbalimbali. Tumekuwa tukitumia karibu katika vituo vyetu vyote hivi. Kwa hiyo, hakuna separation kwamba kituo hiki kinatumia Akili Mnemba au kituo hiki hakitumii.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika vituo vyetu hivi vya umahiri vyote 13 tumeweza kutumia masuala haya ya Akili Unde au Akili Mnemba kwa namna moja au nyingine. Chuo chetu cha DIT pale Dar es Salaam chenyewe hasa kimejikita kwenye masuala hayo ya TEHAMA kama ni kituo cha umahiri kinachofanya utafiti katika masuala ya TEHAMA.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo la pili, Serikali kupitia Tume yetu ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ndiyo ambayo imepewa mamlaka ya kuratibu masuala haya ya ubunifu na imekuwa ikitoa mafunzo ya mara kwa mara kwenye taasisi zetu za elimu ya juu zile za binafsi na zile za umma.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunavisaidia vituo vyetu hivi vya elimu ya juu vya binafsi kwa kupitia Tume yetu ya Sayansi na Teknolojia pale Dar es Salaam kwa kutoa mafunzo ya mara kwa mara. Hata hivyo, kwenye vituo hivi 13 vya umahiri nilivyovitaja, hata hizi taasisi binafsi zinaruhusiwa kwenda kufanya utafiti na kutumia vifaa vilivyopo kwenye vituo hivi vya umma kwa ajili ya kuendeleza tafiti zao hata zile taasisi zetu binafsi zinaruhusiwa kwenda. Ninakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved