Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 2 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 16 2025-04-09

Name

Jafari Chege Wambura

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rorya

Primary Question

MHE. BONIPHACE M. GETERE K.n.y. MHE. JAFARI W. CHEGE aliuliza:-

Je, kuna mpango gani wa ujenzi wa Stendi Wilayani Rorya ili kuongeza mapato ya halmashauri?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa Wananchi wa Rorya kuwa na Stendi ya Mabasi kwa lengo la kuongeza mapato ya halmashauri na kuboresha huduma za usafiri kwa wananchi. Kwa sababu hiyo, Serikali kupitia halmashauri imetenga eneo la ardhi lenye ukubwa wa ekari 10 katika Kijiji cha Mika na Nyasoko kwa ajili ya ujenzi wa stendi ya Wilaya ya Rorya.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuanza, Halmashauri kupitia mapato ya ndani imetumia shilingi milioni 98 kujenga stendi ya muda katika Kijiji cha Mika ili kuwezesha wananchi kupata huduma ya stendi na kuongeza mapato ya Halmashauri ya Rorya.

Mheshimiwa Naibu Spika, halmashauri imefanya mazungumzo ya awali na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) chini ya Wizara ya Fedha ili kuweza kutekeleza mradi huo wa kimkakati.