Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE K.n.y. MHE. JAFARI W. CHEGE aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa ujenzi wa Stendi Wilayani Rorya ili kuongeza mapato ya halmashauri?
Supplementary Question 1
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, nina maswali mawili katika hili swali namba 16.
Swali la kwanza; Stendi ya Rorya imekuwa na ahadi ya muda mrefu sana, hata Mbunge aliyepita alikuwa na hoja hii hii ya stendi ya Rorya. Je, ni lini sasa Serikali itatizimiza ahadi hiyo ya kuwajengea wananchi wa Rorya stendi yao?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Kijiji cha Nyamuswa, Kata ya Nyamuswa katika Jimbo la Bunda wamejenga Stendi kwa nguvu zao binafsi. Je, ni lini Serikali itawa-support wananchi katika Stendi hiyo ya Mji wa Nyamuswa?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba hitaji la Stendi ya Mabasi ya Kisasa katika Halmashauri ya Rorya ni ya muda mrefu. Hata hivyo, Serikali imekuwa ikichukua hatua; kwanza tuliielekeza halmashauri kutenga eneo lenye ukubwa unaostahili ambapo wamekwishapata eneo la ekari 10.
Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, tayari Serikali imeshapeleka fedha milioni 98 na kujenga stendi ya mabasi kwa hatua za awali. Vilevile, katika mwaka ujao wa fedha tunawasiliana na kufanya mazungumzo na sekta ya mashirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kwa ajili ya kuanza ujenzi huu. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tayari Serikali imeshaweka mipango thabiti kwa ajili ya kwenda kujenga kituo cha mabasi pale Rorya.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, kuhusiana na Stendi ya Nyamuswa, kwanza niwapongeze Wananchi na Serikali ya Kijiji cha Nyamuswa kwa kufanya jitihada za kujenga stendi hiyo. Pia, nimhakikishie kwamba Serikali kupitia mapato ya ndani ya halmashauri au fedha za Serikali Kuu tutakwenda kuunga mkono ujenzi wa stendi hiyo ili uweze kuwa bora zaidi.
Name
Mrisho Mashaka Gambo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arusha Mjini
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE K.n.y. MHE. JAFARI W. CHEGE aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa ujenzi wa Stendi Wilayani Rorya ili kuongeza mapato ya halmashauri?
Supplementary Question 2
MHE. MRISHO M. GAMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Jiji la Arusha liliingia kwenye Mradi wa TACTIC toka mwaka 2023 na Januari, 2024 ilitangazwa tenda kwa ajili ya kujenga Stendi ya kisasa Jiji la Arusha. Hata hivyo, mpaka leo ni mwaka mmoja na miezi mitatu bado mkandarasi hajaenda site. Je, ni lini Serikali itaanza kujenga stendi Jiji la Arusha?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Serikali kupitia Mpango wa TACTIC iliainisha Ujenzi wa stendi ya mabasi katika eneo la Bondeni City katika Jiji la Arusha na tayari taratibu za manunuzi zimekwishafanyika na ziko katika hatua za mwisho kwa ajili ya kuanza utekelezaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, nafahamu Mheshimiwa Mrisho Gambo amefuatilia kwa karibu sana suala la ujenzi wa stendi pale Bondeni City. Ninaomba nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Wananchi wote wa Jiji la Arusha, kwamba, Serikali wakati wowote kuanzia sasa itaanza ujenzi wa stendi pale Bondeni City. Ahsante sana.
Name
Dr. Christina Christopher Mnzava
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE K.n.y. MHE. JAFARI W. CHEGE aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa ujenzi wa Stendi Wilayani Rorya ili kuongeza mapato ya halmashauri?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. CHRISTINA C MNZAVA: Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Stendi ya Kahama?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilishaweka Mpango wa kuainisha maeneo yanayohitaji stendi. Pia, katika Miji, Majiji na Manispaa, tulishatoa maelekezo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kuainisha maeneo yanayofaa kwa ajili ya ujenzi wa stendi na kuandaa fedha za mapato ya ndani au kuandika miradi ya kimkakati na kuwasilisha Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Wizara ya Fedha kwa ajili ya ujenzi wa stendi hizo.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, kumwelekeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, kuandaa andiko hilo na kuwasilishwa Ofisi ya Rais, TAMISEMI, lakini pia kuanza kutenga mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa stendi hizo. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved