Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 2 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 17 2025-04-09

Name

Juliana Daniel Shonza

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya katika Kata ya Luswisi?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kujenga vituo vya kutolea huduma za afya kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini. Katika kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2023/2024 jumla ya vituo vya afya 367 vimejengwa na vinatoa huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Luswisi ipo umbali wa takribani kilometa tano kutoka Kituo cha Afya cha Lubanda na idadi ya wananchi wapatao 4,155 kati ya angalau 10,000 wanaohitajika kwa mujibu wa vigezo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendeea kujenga vituo vya afya katika kata za kimkakati kote nchini zikiwemo kata zitakazokidhi vigezo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje.