Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Juliana Daniel Shonza
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya katika Kata ya Luswisi?
Supplementary Question 1
MHE. JULIANA D. SHONZA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; wananchi wa Kata ya Kalembo wameanzisha ujenzi wa Kituo cha Afya, ninaomba kufahamu ni lini Serikali itapeleka hizo fedha ili kuweza kumalizia hicho kituo cha afya?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; Kata ya Malangali na Kata ya Kafule hazina Vituo vya Afya, ninaomba kufahamu ni lini Serikali itapeleka fedha ili vituo hivyo vya afya viweze kujengwa na akinamama wa kata hizo waweze kuondokana na changamoto ya afya? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niwapongeze wananchi wa kata hiyo ambayo Mheshimiwa Juliana Shonza ameitaja ambao wameanza kwa nguvu zao kujenga kituo cha afya. Niwahakikishie kabisa kwamba dhamira ya Serikali hii ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kusogeza huduma za afya karibu na wananchi na tutahakikisha tunatafuta fedha aidha kupitia mapato ya ndani ya halmsahauri au kupitia Serikali Kuu kwenda kukamilisha ujenzi wa kituo hicho cha afya.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili kuhusiana na kata hizo mbili ambazo hazina vituo vya afya, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tutawasiliana na halmashauri hizo ili kuweza kuona kama kata hizo zinakidhi vigezo kwa maana ya idadi ya wananchi na umbali kutoka kituo cha jirani zaidi, lakini pia hali ya kijiografia na ikiwa inakidhi vigezo tutaziweka katika mpango wa ujenzi kwa awamu. Ahsante sana.
Name
Suma Ikenda Fyandomo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya katika Kata ya Luswisi?
Supplementary Question 2
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Wilaya ya Kyela iliyopo kwenye Mkoa wa Mbeya ina Vituo vya Afya vinne ambavyo havijamaliziwa ujenzi wake, viko kwenye Kata ya Itope, Njisi, Ngonga na Makwale. Je, ni lini sasa Serikali italeta fedha za kumalizia ujenzi wa vituo hivyo? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama alivyouliza Mheshimiwa Suma Fyandomo, kwamba Vituo vya Afya katika Kata hizo za Njisi, Itope, Makwale na Ngonga vilianza na ujenzi na Serikali ilishapeleka fedha na tunafahamu kwamba vimejengwa kwa awamu ya kwanza.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwamba, ujenzi wa vituo vyetu vya afya tunakwenda kwa awamu. Tuna awamu ya kwanza ya majengo yale matano ya kwanza, lakini tutakwenda awamu ya pili kwa ajili ya majengo yote yanayosalia. Kwa hiyo, nimhakikishie Mbunge pamoja na wananchi wa Kyela, kwamba, vituo hivyo vya afya vitawekwa kwenye mpango kwa ajili ya kukamilisha majengo hayo. Ahsante sana.
Name
Esther Lukago Midimu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya katika Kata ya Luswisi?
Supplementary Question 3
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Kata ya Laini, Wilaya ya Itilima ina wakazi wengi na haina kituo cha afya. Je, ni lini Serikali itajenga Kituo cha Afya katika Kata ya Laini?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kuandaa mpango mkakati wa ujenzi wa vituo vya afya katika kata zote za kimkakati, tulipitia halmashauri zote 184 ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Itilima. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tutakwenda kutenga bajeti kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kituo hicho cha afya ikiwa kinakidhi ambavyo vimewekwa kwa mujibu wa mwongozo. Ahsante sana.
Name
Jonas William Mbunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbinga Mjini
Primary Question
MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya katika Kata ya Luswisi?
Supplementary Question 4
MHE. JONAS W. MBUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Serikali ilitoa shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Myangayanga. Ni lini sasa Serikali itatoa fedha kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Kituo hicho kinakamilika?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama alivyosema Mheshimiwa Jonas, katika Jimbo la Mbinga Mjini tulishatoa fedha milioni 250, kwa ajili ya kituo hicho cha afya na tutapeleka milioni 250 nyingine katika mwaka ujao wa fedha 2025/2026 kwa ajili ya kukamilisha majengo yaliyosalia. Ahsante sana.
Name
Dr. Charles Stephen Kimei
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vunjo
Primary Question
MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya katika Kata ya Luswisi?
Supplementary Question 5
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha OPD Himo, kilipandishwa hadhi ya kuwa kituo cha afya mwaka 2020 na kuahidiwa majengo ya mortuary, upasuaji na maabara. Mpaka leo kituo hicho kinatoa huduma kama kituo cha afya lakini majengo hayo hayajapatikana. Je, ni lini majengo hayo yatapatikana?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Dkt. Charles Kimei amefuatilia mara kadhaa na ameuliza mara kadhaa hapa Bungeni na Serikali tulimjibu na kumhakikishia kwamba tumekwishaingiza kwenye mpango wa Benki ya Dunia ili kuhakikisha kwamba fedha zinapelekwa kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo kwenye kituo hicho cha afya.
Mheshimiwa Naibu Spika, tayari tuko kwenye hatua za mwisho sana na tumeshapeleka orodha hiyo Wizara ya Fedha na wenzetu wa Wizara ya Fedha wakati wowote watatoa fedha hizo kwa ajili ya kuanza ujenzi wa majengo hayo katika kituo hicho cha afya.
Name
Joseph Kasheku Musukuma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Geita
Primary Question
MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya katika Kata ya Luswisi?
Supplementary Question 6
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Afya cha Bugarama kilichopo Jimbo la Geita kililetewa milioni 475 za tozo na bajeti ilikuwa milioni 600, balance milioni 125. Ninataka kujua, je, ni lini milioni 125 italetwa ili kiweze kukamilika na kuanza kazi? Ninakushukuru.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Afya cha Bugarama, katika Halmashauri ya Geita Vijijini kimewekwa kwenye bajeti ya 2025/2026 na nimhakikishie Mheshimiwa Musukuma kwamba fedha hiyo itapelekwa na tutakamilisha majengo hayo yaliyobakia kwa maana ya milioni 125.
Name
Jesca Jonathani Msambatavangu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Primary Question
MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Afya katika Kata ya Luswisi?
Supplementary Question 7
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Afya Ipogolo na Kituo cha Afya Ngome ni vituo vya zamani sana. Ni lini Serikali itatuletea fedha kwa ajili ya kujenga combined Maternity ward? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, viko vituo vya afya ambavyo ni vikongwe na chakavu vikiwemo vituo vya afya ambavyo Mheshimiwa Mbunge amevitaja vya Ipogolo na Ngome. Hata hivyo, kwanza tuliweka mpango wa ukarabati wa Hospitali za Halmashauri 91, tumeshakarabati 50 kwa maana ya kipaumbele cha kwanza na baada ya hapo tutakwenda kwenye kipaumbele cha vituo vya afya. Kwa hiyo, nikuhakikishie Mbunge, kwamba, kwa sababu tayari tumeshaainisha vituo vya afya takribani 252 vikiwemo hivyo kwa ajili ya ukarabati na tutafanya ukarabati huo.