Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 2 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 18 2025-04-09

Name

Dr. Florence George Samizi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza:-

Je, lini Mabweni ya Sekondari ya Busagara na Kumgogo – Muhambwe yatajengwa ili kuanza kidato cha tano na sita?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2023/2024 Serikali ilipeleka shilingi milioni 680 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni katika Shule za Sekondari Busagara (mabweni matatu) na Kumgogo (mabweni mawili).

Mheshimiwa Naibu Spika, Shule za Sekondari Busagara na Kumgogo zimeanza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano mwaka 2024 ambapo Shule ya Sekondari Busagara ilipangiwa wanafunzi 88 na Shule ya Sekondari Kumgogo ilipangiwa wanafunzi 93.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya shule za sekondari zikiwemo Shule za Busagara na Kumgogo kadri ya upatikanaji wa fedha.