Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kavejuru Eliadory Felix

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buhigwe

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza:- Je, lini Mabweni ya Sekondari ya Busagara na Kumgogo – Muhambwe yatajengwa ili kuanza kidato cha tano na sita?

Supplementary Question 1

MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, kwanza nipongeze na kushukuru. Nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Shule za Sekondari Muhinda, Muzeze katika Jimbo la Buhigwe, zipo kwenye Mchakato wa kupandishwa hadhi ili ziwe na “A”Level. Je, ni lini mchakato huo utakamilika?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake zuri ambalo ana nia ya kufuatilia ustawi wa Sekta ya Elimu katika jimbo lake. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwa sababu Serikali tayari imeanza kufanya tathmini katika shule alizozitaja kwa ajili ya kuona kama zinakidhi vigezo kupandishwa hadhi. Pia, Serikali inaweka kwenye mipango na bajeti yake kupitia Halmashauri ili iweze kuanza kujenga shule hizo kwa maana ya kujenga mabweni kwa ajili ya hatimaye kuja kupandishwa hadhi shule hizo kuwa form five na form six. (Makofi)

Name

Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza:- Je, lini Mabweni ya Sekondari ya Busagara na Kumgogo – Muhambwe yatajengwa ili kuanza kidato cha tano na sita?

Supplementary Question 2

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilituletea takribani shilingi milioni 470 kwa ajili ya Shule ya Sekondari Sayuta ili iweze kupandishwa hadhi na kuwa shule ya kidato cha tano na cha sita, lakini bahati mbaya ni kwamba bweni la wavulana limejengwa, lakini halijakamilika na tuna uhitaji kama shilingi milioni 30. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yupo tayari kutoa maelekezo tupate kiasi hicho ili shule iweze kuanza? (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake hili zuri kabisa ambalo linalenga kuhakikisha Sekta ya Elimu inaboreshwa katika jimbo lake. Nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kumuagiza Mkurugenzi aweze kutenga fedha kupitia mapato ya ndani ya halmashauri kiwango cha shilingi milioni 30 ili aweze kukamilisha miundombinu ambayo inahitajika kwa ajili ya shule hii kuanza kutumika.

Name

Dr. Oscar Ishengoma Kikoyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba kusini

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza:- Je, lini Mabweni ya Sekondari ya Busagara na Kumgogo – Muhambwe yatajengwa ili kuanza kidato cha tano na sita?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Shule ya Sekondari Mazinga ambayo ni shule ambayo iko katikati ya Ziwa Victoria, watoto ili waende shule lazima wapande boats na kipindi cha mvua na wakati wa upepo mkali hawawezi kwenda. Je, ni lini Serikali itatupatia pesa ya kujenga mabweni kwenye hiyo shule ili watoto wetu waweze kusoma? (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimpongeze sana Mheshimiwa Dkt. Kikoyo kwa swali lake hili zuri. Ninaomba nimtaarifu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ya Awamu ya Sita imeweza kufanya uwekezaji wa jumla ya shilingi trilioni 5.1 katika Sekta ya Elimu kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika shule za msingi na shule za sekondari.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha Awamu hii ya Sita pia yamejengwa mabweni 738 na Serikali bado inaendelea na jitihada hizo.

Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Serikali kwa kuzingatia mazingira ambayo umeyataja itafika katika jimbo lake kwa ajili ya kuhakikisha shule hiyo inaweza kujengewa bweni ili wanafunzi wetu wapate sehemu nzuri na salama ya kusomea.