Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 2 Public Service Management Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 19 2025-04-09

Name

Maimuna Salum Mtanda

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Newala Vijijini

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza:-

Je, upi utaratibu wa Serikali kuwapandisha madaraja watumishi waliofanya kazi zaidi ya miaka saba bila kupandishwa daraja?

Name

George Boniface Simbachawene

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibakwe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, upandishaji wa vyeo kwa watumishi hufanyika kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyoainishwa katika Miundo ya Maendeleo ya Utumishi ya Kada zao pamoja na mambo yote yaliyoainishwa katika Aya ya 4.4 ya Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma Toleo la Mwaka 2008, Kanuni D.51 (1) na (2) ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma, Toleo la mwaka 2009. Pamoja na sifa na vigezo hivi, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Utumishi ana mamlaka ya kuwapandisha vyeo watumishi wenye sifa waliocheleweshwa kupandishwa cheo kwa mujibu wa Miundo ya Maendeleo ya Utumishi kwa njia ya mserereko kwenye vyeo wanavyostahili.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali imewapandisha vyeo watumishi 1,556 waliocheleweshwa kupandishwa cheo kwa wakati kwa mserereko na mwaka wa fedha 2024/2025 watumishi 4,259. Hivyo, Serikali itaendelea kuwabaini na kuwapandisha vyeo watumishi waliochelewa kupandishwa vyeo na swali hili limeulizwa na Mheshimiwa Maimuna Salum Mtanda, Mbunge wa Newala.