Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Maimuna Salum Mtanda

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Newala Vijijini

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza:- Je, upi utaratibu wa Serikali kuwapandisha madaraja watumishi waliofanya kazi zaidi ya miaka saba bila kupandishwa daraja?

Supplementary Question 1

MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa fursa hii na nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwenye Jimbo la Newala Vijijini wapo watumishi ambao walipata athari za kutopandishwa vyeo kwa wakati kipindi kile cha uhakiki wa watumishi ambacho kilifanyika mwaka 2016 mpaka 2018. Watumishi hao mpaka leo bado wanalalamika hawajapanda vyeo. Je, upi mpango wa Serikali wa kuwanusuru watumishi hawa ili waende sambamba na wenzao?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; ninaomba Kiti chako kione namna ya kuwakwamua wale wote ambao walikwama kupandishwa madaraja kwa utaratibu wa kawaida ili waweze kuungana na wenzao wawekwe kwenye kundi moja kwa sababu sasa hivi wamepitwa hata na wale ambao waliajiriwa nyuma yao. Kwa hiyo ninaomba Serikali ione namna ambavyo itawafanya watu hawa wawe katika usawa na wenzao wale ambao walipandishwa vyeo huko nyuma bila kupata mkwamo. Ninakushukuru.

Name

George Boniface Simbachawene

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibakwe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba kuna kipindi ambacho upandishwaji wa madaraja kwa watumishi ulisimama na hivyo njia pekee ya kuweza kufanya hivyo ilikuwa ni kuwapandisha kwa mserereko. Serikali imekuwa ikifanya hivyo na ndiyo maana nimesema watumishi 1,556 waliweza kupandishwa na tumeendelea kufanya hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, shida moja ambayo inatokea ni kwa waajiri wetu wanapochelewa kuweka data zao vizuri kwa rekodi za watumishi na kuomba Wizarani kwetu ili tuweze kuchukua hatua hiyo. Hata hivyo, kuna kipindi cha mwaka 2023/2024, bajeti tuliyokuwa tumepanga kwa ajili ya kupandisha vyeo ilibaki kwa sababu hawakuweza kuleta watu wanaotakiwa. Kwa hiyo nitoe rai kwa Halmashauri zetu, waajiri wetu na waajiri wengine kuhakikisha kwamba wanaleta majina ya watumishi wanaotaka wapandishwe vyeo kwa mserereko ili maombi hayo tuyashughulikie kwa pamoja na hili ni kwa nchi nzima.

Name

Janejelly Ntate James

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza:- Je, upi utaratibu wa Serikali kuwapandisha madaraja watumishi waliofanya kazi zaidi ya miaka saba bila kupandishwa daraja?

Supplementary Question 2

MHE. JANEJELLY J. NTATE: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na juhudi za Serikali mnazofanya kwa upandishaji wa vyeo, lakini ili mtumishi afanyiwe ukokotozi wa kikokotoo chake ni lazima hicho cheo awe amekaa nacho si chini ya miezi sita. Je, hawa watumishi waliocheleweshwa na wengine wamebakiza mwezi kustaafu, wengine wanastaafu leo, Serikali itawachukulia vipi kwenye kikokotozi chao? (Makofi)

Name

George Boniface Simbachawene

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibakwe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Janejelly kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kikokotoo kinazingatia sana ule muda aliopandishwa cheo mtumishi. Hata hivyo, tumekuwa kama Serikali tukiwashughulikia zaidi wale wanaokaribia kustaafu na kuhakikisha kwamba mambo yao yamekaa sawa. Shida moja inakuja tu pale ambapo waajiri hawafanyi kazi ile kwa wakati hata mpaka unakuta wakati hesabu inapigwa sasa bado mtumishi yule mwajiri wake hajaleta taarifa zake ipasavyo. Kwa hiyo tusaidiane wote sisi na waajiri tumewapa maelekezo kwamba wahakikishe wale wanaokaribia kustaafu basi taarifa zao zinakuja ili tuweze kuwawekea hesabu zao sawasawa ili zisiathiri maslahi yao ya kustaafu.

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza:- Je, upi utaratibu wa Serikali kuwapandisha madaraja watumishi waliofanya kazi zaidi ya miaka saba bila kupandishwa daraja?

Supplementary Question 3

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Mheshimiwa Waziri kumekuwa na mkwamo mkubwa sana kwa wafanyakazi ambao wameongeza elimu wakiwa kazini kuweza kubadilishiwa madaraja au kuhamishiwa kwenye lile somo alilosomea. Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia walimu hao au wafanyakazi wa aina hiyo?

Name

George Boniface Simbachawene

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibakwe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kumekuwa na changamoto kwenye eneo hilo, lakini kwa sehemu fulani linachangiwa pia na watumishi wenyewe. Mtumishi ameruhusiwa na mwajiri wake akasome kitu hiki akienda kule anasoma kitu kingine ambacho pengine kinaweza kikahusisha re-categorization ili mambo yake mengine yaweze kuendelezwa. Sasa inapotokea mkanganyiko kama huo inakuja issue ya ushirikiano kati ya Wizara ya Utumishi pamoja na mwajiri na mtumishi mwenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, hapo ninadhani tutaendelea kulishughulikia hili. Kwa upande wa Serikali tumekuwa tukifanya re-categorization sikumbuki takwimu, lakini pia tumekuwa tukitambua nafasi zao na elimu walizozisomea kwa wakati ili mtumishi aweze kupata motisha na kuendelea kufanya kazi vizuri. Hata hivyo, baadhi kwa kweli wanakwamishwa na waajiri wao kutokuwa active katika kuleta taarifa kwetu sisi kwa sababu kwetu sisi tunapokea taarifa kutoka kwa mwajiri na siyo kutoka kwa mtumishi mwenyewe.