Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 2 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 24 2025-04-09

Name

Abubakar Damian Asenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilombero

Primary Question

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itatimiza ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Kilombero?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kilombero ulianza mwezi Juni, 2024. Ujenzi umefika kwenye hatua ya umaliziaji na hadi sasa Serikali imeshatoa kiasi cha fedha shilingi 651,000,000 kwa ajili ya ujenzi huo. Kazi zinazoendelea kufanyika kwa sasa ni kuweka sakafu ya vigae, dari ya jasi, kuweka vioo kwenye madirisha na kupaka rangi. Ahsante. (Makofi)