Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Abubakar Damian Asenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilombero
Primary Question
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza:- Je, lini Serikali itatimiza ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Kilombero?
Supplementary Question 1
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kuishukuru Serikali hapa na kama ulivyosema jana kwamba Serikali iko kazini, ninathibitisha majibu haya ya Serikali kwamba Kituo cha Polisi kimejengwa na kimeshafikia 85% na mpaka viyoyozi vimeshanunuliwa. Ninaomba kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa sababu ni Kituo cha Polisi cha Wilaya, je, Serikali ina mpango gani wa kujenga uzio na nyumba za Polisi?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; mwaka 2023 Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani alitembelea Jimbo la Kilombero na Kata ya Mwaya, akatembelea kituo cha Polisi cha mabanzi ya mbao na akaahidi kwamba ataleta pesa za kujenga Kituo cha Polisi cha Kata ya Mwaya. Je, ni lini Serikali itatimiza ahadi hiyo? Ahsante. (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninachukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Asenga kwa ufuatiliaji mzuri wa kituo hicho cha Polisi ambacho kimefikia hatua nzuri ya 85%. Ninaomba kujibu maswali mawili kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Jeshi la Polisi litafanya tathmini ya gharama ya uzio pamoja na nyumba ya OCS, tayari kwa ajili ya kujenga nyumba hizo ili kuziweka kwenye mpango, kutengewa fedha na kuanza kujengwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu ahadi ya Serikali ya mwaka 2023, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge, Serikali imekuwa ikiahidi na kutekeleza. Katika Kata ya Mwaya ambayo ameitaja tutaiweka kwenye mpango na kutengewa fedha, tayari kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Kata ya Mwaya. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Emmanuel Peter Cherehani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ushetu
Primary Question
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza:- Je, lini Serikali itatimiza ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Kilombero?
Supplementary Question 2
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Naibu Spika, nimekuwa nikiahidiwa kila bajeti, juu ya ujenzi wa Kituo cha Polisi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu. Sasa ninaomba nipate commitment ya Serikali, ni lini ujenzi huu utaanza? Ahsante sana.
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Cherehani kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ninakumbuka tarehe 5 Aprili, 2024 nilijibu swali la msingi la Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mwaka wa fedha 2025/2026, tunaenda kutenga fedha na kujenga Kituo cha Polisi cha Ushetu. Ahsante sana.
Name
Hassan Zidadu Kungu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduru Kaskazini
Primary Question
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza:- Je, lini Serikali itatimiza ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Kilombero?
Supplementary Question 3
MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa nafasi. Kata ya Matemanga haina kabisa kituo kidogo cha Polisi na Polisi wale wanafanya kazi katika chumba ambacho walipewa kwenye jengo lililoachwa na wakandarasi wa barabara. Je, ni lini Serikali itatupatia fedha ya kwenda kujenga Kituo Kidogo cha Polisi katika Kata ya Matemanga? Ahsante. (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Hassan kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inajenga vituo vya Polisi kwenye Kata zote ila inajenga awamu kwa awamu. Kwa hiyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa Kata ya Matemanga ambayo ameitaja, tutaiweka kwenye mpango na kutengewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi kwenye Kata hiyo aliyoitaja. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved