Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 2 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 25 2025-04-09

Name

Emmanuel Peter Cherehani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Primary Question

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Skimu ya Umwagiliaji katika Jimbo la Ushetu? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Ushetu na Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu lina mabonde mengi yaliyoainishwa kufaa kwa kilimo cha umwagiiliaji ikiwemo Ulowa, Kisuke, Bulugwa, Butibu, Nimbo, Nyamilangano, Sabasabini, Chona, Chambo, Mpunze, Mwadui na Bugomba B.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeanza kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa mabwawa na skimu za umwagiliaji katika Mabonde ya Kisuke, Nimbo na Bulugwa, Butibu kupitia mshauri elekezi ikiwa ni hatua ya kwanza kabla ya kuanza ujenzi. Aidha, kukamilika kwa kazi hii kutasaidia kujua gharama halisi za utekelezaji wa mradi.