Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Emmanuel Peter Cherehani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ushetu
Primary Question
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Skimu ya Umwagiliaji katika Jimbo la Ushetu? (Makofi)
Supplementary Question 1
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana. Pia, ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Ni kweli timu ya wataalam imeshafika na Mheshimiwa Waziri pia alifika. Ninaendelea kuipongeza Serikali lakini ombi langu ni kwamba miradi hii ikamilike kwa wakati ili wananchi wetu wa Jimbo la Ushetu na wanaozunguka maeneo haya ya umwagiliaji waweze kupata manufaa. (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninamthibitishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, yote ambayo Serikali tunaahidi kupitia Wizara ya Kilimo tutayatekeleza kwa wakati. Ahsante. (Makofi)
Name
Leah Jeremiah Komanya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Meatu
Primary Question
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Skimu ya Umwagiliaji katika Jimbo la Ushetu? (Makofi)
Supplementary Question 2
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, Je, ni lini Serikali itachimba kisima katika Kijiji cha Mwamanongu, Kata ya Mwamanongu kwa kuwa tayari wananchi wameshatenga heka 150 kama mpango ulivyo? Ninakushukuru. (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, Wizara ya Kilimo tayari tumeshanunua magari manne kwa ajili ya uchimbaji wa visima katika maeneo yote ambayo tumeyalenga kuwasaidia wakulima. Kwa hiyo, mawili yameshafika na mawili yako njiani, kwa hiyo, tutaanza pamoja na Meatu. Ahsante. (Makofi)
Name
Joseph Michael Mkundi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukerewe
Primary Question
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Skimu ya Umwagiliaji katika Jimbo la Ushetu? (Makofi)
Supplementary Question 3
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninataka kujua ni hatua ipi imefikiwa na Serikali kwa Miradi wa Umwagiliaji ya Kikongola, Bugolola na Miyogwezi ambayo ilitangazwa mwishoni mwa mwaka jana. Ninashukuru. (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwamba, katika miradi ambayo ipo katika Jimbo la Ukerewe, Wizara ya Kilimo hatua tuliyopo sasa hivi ni kwamba, tumeomba fedha Wizara ya Fedha, zikishafika sasa tutapeleka advance payment katika maeneo yote ambayo tayari tulishasaini mikataba na ambayo zipo hatua za mwisho. Ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ilemela
Primary Question
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Skimu ya Umwagiliaji katika Jimbo la Ushetu? (Makofi)
Supplementary Question 4
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Ilemela kama lilivyo Jimbo la Ushetu, linayo mabonde mazuri kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, bahati nzuri Wizara ya Kilimo ilishakuja kufanya upembuzi yakinifu katika Kata ya Nyamhongolo, eneo la Nyamadoke na Kata ya Sangabuye, eneo la Igalagala na wakakamilisha upembuzi huo. Je, ni lini sasa kazi ya kuchimba visima kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji wa mbogamboga utakamilika ili wale watu waweze kufanya kazi yao vizuri? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwamba, kama nilivyojibu katika jibu la Mbunge wa Ushetu, tutafanya vivyo hivyo na Ilemela. Tayari magari tunayo na sasa hivi hatua iliyopo Wizara ya Kilimo ni kwamba, wanakwenda kufanya surveys kwa ajili ya kupata urefu wa maji ili yale magari tuliyonayo yaweze kuelekea katika maeneo yenu. Kwa hiyo, mambo hayo yataanza kuanzia mwaka huu wa fedha na mwaka ujao. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Cecilia Daniel Paresso
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Skimu ya Umwagiliaji katika Jimbo la Ushetu? (Makofi)
Supplementary Question 5
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Bonde la Eyasi katika Wilaya ya Karatu kuna mradi wa ujenzi wa skimu ya umwagiliaji, mradi ule una thamani ya shilingi bilioni 21, lakini mradi ule umesimama kwa muda mrefu karibu mwaka mzima. Je, ni nini kilichosababisha mradi huo usimame na ni lini utaratibu wa kukamilisha skimu hizo utaendelea? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli anachoeleza Mheshimiwa Mbunge kwamba, Mradi wa Bonde la Eyasi thamani yake ni shilingi bilioni 21.8 na tayari sisi kama Serikali tumeshatoa shilingi bilioni 6.4 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo, Mkandarasi anaendelea na kazi iliyoko pale. Kulikuwa tu na changamoto zikiwemo za mvua, lakini vilevile tumeshakubaliana kwamba atarudi site kumalizia ile kazi kwa wakati, kwa sababu fedha iliyopo inatosha kwenda zaidi ya asilimia 30 ya kazi. Ahsante sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved