Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 2 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 27 2025-04-09

Name

Silvestry Fransis Koka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibaha Mjini

Primary Question

MHE. JACKSON G. KISWAGA K.n.y. MHE. SILVESTRY F. KOKA aliuliza:-

Je, lini Serikali itaendeleza upanuzi wa Barabara kipande cha Kibaha – Chalinze kuwa njia nane ili kuondoa msongamano wa magari Kibaha?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali haitaendeleza upanuzi wa Barabara sehemu ya Kibaha – Chalinze, badala yake Serikali itajenga Express Way ya kutoka Kibaha – Chalinze – Morogoro (kilometa 220) kwa utaratibu wa ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (Public Private Partnership (PPP)). Kwa sehemu ya Kibaha – Chalinze, zabuni ya kumpata mwekezaji iko katika hatua ya mwisho ya majadiliano. Ujenzi unatarajiwa kuanza baada ya majadiliano kukamilika na mkataba (Concession Agreement) kusainiwa.