Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jackson Gedion Kiswaga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalenga
Primary Question
MHE. JACKSON G. KISWAGA K.n.y. MHE. SILVESTRY F. KOKA aliuliza:- Je, lini Serikali itaendeleza upanuzi wa Barabara kipande cha Kibaha – Chalinze kuwa njia nane ili kuondoa msongamano wa magari Kibaha?
Supplementary Question 1
MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Koka ninaishukuru Serikali kwa mkakati huo, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; kwanza naishukuru sana Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Jimbo la Kalenga inajenga barabara tatu za lami, lakini imejenga Barabara kutoka Wenda – Mgama, sasa kutoka Mgama kwenda pale Iheme kuna kilometa sita. Je, ni lini Serikali itatusaidia na hicho kipande cha kilometa sita kijengwe?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Serikali inajenga Barabara kutoka Tosamaganga kwenda Ugwachanya, kuna kipande kama cha mita 900 na kilikuwa katika mpango wa kujengwa mwaka huu. Je, lini Serikali itatupelekea fedha ili tuweze kukamilisha hicho kipande? Ahsante sana.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nijibu maswali yote mawili kwa pamoja. Dhamira ya Serikali, kama alivyosema Mheshimiwa, ni kujenga hiyo Barabara ya Wenda – Mgama na Tosamaganga kwa kiwango cha lami. Kwa hiyo, ujenzi wake utategemea na upatikanaji wa fedha ambayo ndio dhamira ya Serikali kuzijenga barabara hizo kwa kiwango cha lami. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved