Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 2 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 28 2025-04-09

Name

Subira Khamis Mgalu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. LEAH J. KOMANYA K.n.y. MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza:-

Je, lini ujenzi wa Daraja la Mpiji Chini, Kata ya Mapinga, utakamilika?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) itajenga Daraja la Mpiji kupitia Mpango wa Matengenezo ya Dharura yanayogharamiwa kwa fedha za mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia, kupitia Crisis Response Window. Kwa sasa taratibu za manunuzi ya kumpata mkandarasi wa ujenzi wa daraja hilo zinaendelea na mara baada ya kukamilika ujenzi utaanza. Ahsante.