Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Leah Jeremiah Komanya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Meatu
Primary Question
MHE. LEAH J. KOMANYA K.n.y. MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Daraja la Mpiji Chini, Kata ya Mapinga, utakamilika?
Supplementary Question 1
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu ya Serikali, lakini nina maswali mawili. Swali la kwanza; je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Daraja la Itembe lililopo Jimbo la Meatu?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; je, lini Serikali itaanza ujenzi wa madaraja katika Mto Chobe, Liusa na Nkoma?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, Daraja la Itembe lipo kwenye barabara kubwa ya kutoka Maswa, kuja Sibiti, kuja Singida na Mheshimiwa Mbunge ni shahidi kwamba, tuko kwenye asilimia za juu kabisa katika ujenzi. Kitu ambacho sasa hivi tunafanya, tumeshapokea certificate ya mkandarasi, ili aweze kulipwa na kuendelea na kazi na tunatamani kazi hiyo ikamilike mapema iwezekanavyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu madaraja mengine aliyoyataja, Serikali ina mpango wa kuyajenga, lakini itategemea na upatikanaji wa fedha. Ahsante sana.
Name
Ally Mohamed Kassinge
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kusini
Primary Question
MHE. LEAH J. KOMANYA K.n.y. MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Daraja la Mpiji Chini, Kata ya Mapinga, utakamilika?
Supplementary Question 2
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Naibu Spika, je, ujenzi wa Daraja la Mto Nakiu kutoka Nanjirinji kuelekea Ruangwa lini utakamilika? Ninakushukuru.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa hilo daraja bado haujaanza, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, ni kati ya madaraja ambayo yako kwenye mpango wa madaraja ya dharura ambapo wenzetu wa World Bank watatukopesha na tayari hizo fedha tumeshazipata. Kwa hiyo, tuwe na uhakika kwamba, daraja hilo linaenda kukamilika. Ahsante.
Name
Dr. John Danielson Pallangyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Mashariki
Primary Question
MHE. LEAH J. KOMANYA K.n.y. MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Daraja la Mpiji Chini, Kata ya Mapinga, utakamilika?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa hii nafasi. Je, ni lini Daraja la Mto Kikavu litajengwa upya pamoja na kuipanua Barabara ya Moshi – Arusha, ambapo sasahivi kuna msongamano mkubwa kati ya Moshi mpaka Sangisi?
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, sijamsikia vizuri daraja alilolitaja na barabara yake.
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Naibu Spika, narudia. Je, ni lini Serikali itakwenda kujenga upya Daraja la Mto Kikavu katika Barabara ya Moshi – Arusha, pamoja na kuipanua barabara ile kuanzia Sangisi – Tengeru mpaka Moshi kwa sababu, sasahivi ina msongamano mkubwa wa magari? Ahsante.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli, Daraja la Kikavu kwanza lilipo linahamishwa na itajengwa kwa njia nne na tunajenga kupitia Mfuko wa JICA ambao usanifu umeshakamilika. Muda wowote tunategemea kazi hiyo ya kupanua hiyo barabara na kulijenga daraja hilo upya ianze. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved