Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 2 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 30 2025-04-09

Name

Mariam Madalu Nyoka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM M. NYOKA aliuliza:-

Je, Serikali imejipangaje kutoa elimu ya mikopo ya Mifuko mbalimbali inayokopesha makundi maalum?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inaendelea kushirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Ofisi za Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Halmashauri na viongozi wa wafanyabiashara ndogondogo tunaendelea kuhamasisha na kutoa elimu kwa umma kupitia mikutano ya hadhara, vyombo vya habari na watu mashuhuri kupitia majukwaa yao kutoa elimu juu ya uwepo wa mikopo yenye masharti nafuu inayotolewa na Serikali kwa makundi maalum. Ahsante.