Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mariam Madalu Nyoka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM M. NYOKA aliuliza:- Je, Serikali imejipangaje kutoa elimu ya mikopo ya Mifuko mbalimbali inayokopesha makundi maalum?

Supplementary Question 1

MHE. MARIAM M. NYOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, ipo Mifuko mingapi hadi sasa ambayo ina lengo la kukopesha kundi hili?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; je, Serikali haioni haja ya kuunganisha Mifuko hii ili kuwa na uratibu mzuri zaidi hasa kwa kundi hili maalum? (Makofi)

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mariam, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa swali lake la kwanza; Serikali ina idadi ya Mifuko 75 ambayo inawezesha wananchi kuendeleza kiuchumi na kwa mikopo ya bei nafuu. Katika Mifuko hiyo tuna Mifuko ya 10% ambayo ni mapato ya halmashauri, tuna Mifuko ya Wafanyabiashara Ndogondogo (Machinga) na vilevile lakini tuna Mfuko wa Uwezeshaji wa Wanawake (WDF). (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa swali lake la pili, Serikali inaendelea na mchakato wa kukusanya pamoja Mifuko hii ili kuendelea kuleta ufanisi zaidi kwa kuhakikisha kwamba wananchi wanapata mikopo ile kwa kunufaika. Pia Serikali inaendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Baraza la Taifa la Uwezeshaji ili kuhakikisha kwamba kazi hiyo inafanyika kwa haraka. Ahsante. (Makofi)