Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 3 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 32 2025-04-10

Name

Amandus Julius Chinguile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nachingwea

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA K.n.y. MHE. AMANDUS J. CHINGUILE aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaipandisha hadhi Mamlaka ya Mji Mdogo Nachingwea kuwa Mamlaka ya Mji?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, uanzishaji wa maeneo ya utawala katika Mamlaka za Serikali za Mitaa hufanyika kwa mujibu wa Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura 287, (Mamlaka za Miji), Sura 288 pamoja na Mwongozo wa Uanzishwaji wa Maeneo ya Utawala wa Mwaka 2014. Mwongozo wa kuanzisha maeneo ya utawala unaanza kwa kusudio kujadiliwa kupitia vikao vya ngazi za msingi, Baraza la Madiwani, Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) na Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC). Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea inashauriwa kufuata utaratibu huo na kuwasilisha Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa, mamlaka nyingi zilizoanzishwa bado zina upungufu wa miundombinu mbalimbali yakiwemo majengo ya utawala na huduma za kijamii, kwa sasa Serikali imeweka kipaumbele katika kuboresha miundombinu iliyopo katika maeneo ya utawala yaliyopo. Ahsante.