Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Justin Lazaro Nyamoga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilolo
Primary Question
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA K.n.y. MHE. AMANDUS J. CHINGUILE aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaipandisha hadhi Mamlaka ya Mji Mdogo Nachingwea kuwa Mamlaka ya Mji?
Supplementary Question 1
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu mazuri, lakini pamoja na hayo, kwa niaba ya Mheshimiwa Chinguile ninayo maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; Mji wa Nachingwea ni mji wa kihistoria na ni mji mkongwe na maombi kwa kufuata taratibu zote yalishawasilishwa mara kadhaa. Je, kwa kuzingatia hadhi ya Mji wa Nachingwea, Serikali haioni ni wakati mwafaka sasa kwa kuipa hadhi ya kuwa na halmashauri kamili kama mji?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; ni sambamba na hilo. Mji wa Ilula uliopo Kilolo na wenyewe una zaidi ya miaka 15 ukiwa ni mamlaka ya mji mdogo. Je, hii miji ambayo imekuwa na Mamlaka ya Mji Mdogo kama Ilula, ni lini sasa Serikali itaipa hadhi za kuwa halmashauri kamili?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli, Serikali ilianzisha mamlaka za miji midogo katika halmashauri mbalimbali kote nchini, lakini ili mamlaka zipande hadhi na kuwa halmashauri za miji kamili kuna vigezo ambavyo ni lazima vifikiwe.
Mheshimiwa Naibu Spika, kigezo cha kwanza ni idadi ya wananchi; idadi ya wananchi katika halmashauri inayoanzishwa inatakiwa isipungue watu 150,000 na idadi ya wananchi wanaobaki katika halmashauri mama inatakiwa isipungue wananchi 250,000. Halmashauri ya Nachingwea ina wananchi 233,655, kwa hiyo, hata ikianzisha Halmashauri ya Mji kamili wa Nachingwea bado haitakidhi idadi ya wananchi wanaotakiwa kwa mujibu wa vigezo.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili ni uwezo wa mapato ya ndani; angalau 30% kwa mamlaka inayoanzishwa kuwa halmashauri. Bado Mamlaka ya Nachingwea haina uwezo wa kukidhi kigezo hicho. Kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tunaendelea kuona kwa kadiri ya halmashauri zinavyoendelea kukua na baada ya kukidhi vigezo hivi tutazipandisha hadhi ya kuwa halmashauri za miji kamili.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na Mamlaka ya Mji Mdogo wa Ilula. Kweli ni ya muda mrefu, lakini tumeshapokea maombi kutoka Mkoa wa Iringa na tunaendelea na tathmini ya kuona kama inakidhi vigezo hivyo, ili iweze kupanda hadhi hapo mamlaka itakaporidhia kuanza kupandisha hadhi mamlaka za miji midogo kuwa halmashauri. Ahsante.
Name
Aida Joseph Khenani
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Nkasi Kaskazini
Primary Question
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA K.n.y. MHE. AMANDUS J. CHINGUILE aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaipandisha hadhi Mamlaka ya Mji Mdogo Nachingwea kuwa Mamlaka ya Mji?
Supplementary Question 2
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya TAMISEMI iliagiza timu kwenda Wilaya ya Nkasi na wakasema Mamlaka ya Mji Mdogo Namanyere tumekidhi vigezo. Leo ni mwaka 2025 kutoka mwaka 2013, kama Wizara inaona haijakidhi vigezo kwa nini wasiifute ili wananchi waendelee kuwa vijijini badala ya gharama wanazozipata kwa upande wa TANESCO?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli zipo mamlaka za miji midogo zilizoanzishwa ambazo mpaka sasa zinakidhi vigezo, kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge anaongelea Mamlaka ya Mji Mdogo katika eneo la Halmashauri ya Nkasi.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie Mbunge kwamba, kupanga ni kuchagua na Serikali tumepanga kuanza na vipaumbele vya kukamilisha miundombinu kwenye halmashauri zilizopo. Tunafahamu zipo halmashauri hazina ofisini za wakurugenzi, zipo halmashauri za miji hazina majengo ya utawala na majengo ya huduma za kijamii. Tukaona ni busara kwanza kuanza na hayo majengo yakamilike na baadaye tutakuja kuanza kupandisha halmashauri zote ambazo zimekidhi vigezo. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, zoezi hilo litaendelea muda utakapofika na watapa haki yao ya kuwa na halmashauri ya mji. Ahsante sana.
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Primary Question
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA K.n.y. MHE. AMANDUS J. CHINGUILE aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaipandisha hadhi Mamlaka ya Mji Mdogo Nachingwea kuwa Mamlaka ya Mji?
Supplementary Question 3
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini Serikali itapandisha hadhi Mamlaka ya Mji Mdogo wa Vwawa kuwa Halmashauri ya Mji kwa kuwa, umekidhi vigezo vyote? Ahsante sana.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo nimejibu kwenye majibu yangu ya msingi kwamba, tunafahamu zipo mamlaka ambazo zimekidhi vigezo, lakini tumeweka kipaumbele kuboresha miundombinu ya utawala katika halmshauri zilizopo na baada ya hapo tutakwenda kuanza kupandisha hizo halmashauri nyingine. Kwa hiyo, nimwombe Mheshimiwa Hasunga, wao wawe wavumilivu na kwamba, muda ukifika basi Serikali itaona uwezekano wa kuipandisha halmashauri hiyo.
Name
Dr. John Danielson Pallangyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Mashariki
Primary Question
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA K.n.y. MHE. AMANDUS J. CHINGUILE aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaipandisha hadhi Mamlaka ya Mji Mdogo Nachingwea kuwa Mamlaka ya Mji?
Supplementary Question 4
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa hii nafasi. Mwaka 2012, mwezi Januari, aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete, aliridhia kuigawa Wilaya ya Arumeru ziwe wilaya mbili kwa lengo la kuhakikisha kwamba, wananchi wanapata huduma za utawala kirahisi. Je, Serikali haioni kwamba, sasa ni wakati mwafaka kutekeleza yale aliyoyasema Rais Mstaafu? Ahsante sana.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge Dkt. Pallangyo kwamba, tunatambua zipo halmashauri ambazo zinakidhi vigezo vya kugawa na pia zimeshawasilisha maombi hayo. Ninaomba nikuhakikishie mara tu baada ya kuanza mchakato wa kugawa halmashauri rasmi na baada ya kukamilisha maeneo ambayo tunakamilisha kwa sasa, tutaweka kipaumbele katika Halmashauri ya Arumeru. Ahsante sana.