Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 3 Energy and Minerals Wizara ya Nishati 35 2025-04-10

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO aliuliza:-

Je, Serikali ina maelezo gani juu ya kero sugu ya kukatika umeme mara kwa mara Handeni Mjini na ni lini kero hiyo itatatuliwa?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto ya kukatika umeme Wilayani Handeni inatokana na uchakavu wa miundombinu ya kusambaza umeme pamoja na urefu wa njia za kusambaza umeme. Katika kukabiliana na changamoto hii, Serikali kupitia TANESCO inaendelea na ukarabati wa miundombinu ya umeme, ikiwa ni pamoja na kubadilisha nguzo za miti na kuweka za zege. Aidha, Serikali kupitia Mradi wa Gridi Imara inaendelea na ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Mkata, Handeni ambapo kwa sasa mkandarasi yupo kwenye hatua za awali za ujenzi. Aidha, ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Kilindi umefikia 35% na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 132 kutoka Mkata – Handeni hadi Kilindi umefikia 30%. Kukamilika kwa kazi hizi kutawezesha kuondoa kero sugu ya kukatika umeme Handeni Mjini. Ahsante.