Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO aliuliza:- Je, Serikali ina maelezo gani juu ya kero sugu ya kukatika umeme mara kwa mara Handeni Mjini na ni lini kero hiyo itatatuliwa?

Supplementary Question 1

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; ujenzi huu wa Vituo vya Kupoza Umeme katika eneo la Mkata, Handeni, Lushoto na Kilindi ni muhimu sana kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa umeme katika Mkoa wa Tanga. Hata hivyo, miradi hii inakwenda kwa kusuasua sana. Je, Serikali iko tayari kuharakisha upatikanaji wa fedha ili miradi hii ikamilike kwa wakati?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; njia ya kusafirisha umeme kutoka kituo cha Mkata hadi Kilindi inasuasua kutokana na changamoto ya fidia. Ni kwamba, wale wananchi ambao wamepisha eneo la mradi bado hawajapata fidia. Je, Serikali iko tayari sasa kutoa fidia ili mradi huu ukamilike kwa wakati?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge, kwa maswali mawili mazuri ambayo ameuliza kuhusiana na kuharakisha ujenzi wa Vituo vya Kupoza Umeme vya Mkata, Handeni, Lushoto pamoja na Kilindi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tayari wenzetu wa Wizara ya Fedha wametuhakikishia kuwa watawalipa wakandarasi hawa kwa wakati ili kufanya ujenzi wa vituo hivi vya kupoza umeme uweze kwenda kwa kasi ili wananchi wa Mkoa wa Tanga waweze kunufaika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Lushoto ni Mradi wa Kasiga – Lushoto, ambapo patajengwa njia ya kusafirisha umeme na kituo cha kupoza umeme na tayari tumeshawasiliana na wenzetu wa Wizara ya Fedha na wametuhakikishia kwamba watatupatia fedha kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa vituo hivyo vya kupoza umeme na njia ya kusafirisha umeme ya Kasiga – Lushoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na swali la pili la fidia; fidia ya wananchi ya kujenga njia ya kusafirisha umeme kutoka Mkata, Handeni mpaka Kilindi, ni takribani bilioni 2.63. Pia, tumeshawasiliana na wenzetu wa Wizara ya Fedha na wametuhakikishia watalipa fidia hii kwa sababu ile ya kituo cha kupoza umeme cha Mkata, Handeni tayari imelipwa. Kwa hiyo, tuna uhakika na hii pia italipwa kwa ajili ya kuharakisha ujenzi huu wa njia hii ya kuharakisha umeme ambayo ni muhimu sana kwa maeneo ya Mkata, Handeni pamoja na Kilindi. Ahsante.

Name

Samweli Xaday Hhayuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hanang'

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO aliuliza:- Je, Serikali ina maelezo gani juu ya kero sugu ya kukatika umeme mara kwa mara Handeni Mjini na ni lini kero hiyo itatatuliwa?

Supplementary Question 2

MHE. SAMWEL X. HHAYUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kuniupa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Wilaya ya Hanang ina changamoto kubwa ya umeme kukatika mara kwa mara hivyo kuathiri shughuli za uzalishaji ikiwepo uzalishaji kwenye viwanda. Je, Serikali ina mkakati gani kuondoa adha hii?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, katika Wilaya hii ya Hanang upo Mradi wa Gridi imara wa kujenga kituo cha kupoza umeme kwenye awamu ya pili. Kwa sasa Serikali inaendelea na ujenzi wa awamu ya kwanza ya gridi imara.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mkakati wa kujenga Kituo cha Kupoza Umeme Hanang upo. Ni suala la muda tu kwa sababu mradi huo unatekelezeka kwa awamu. Ahsante.

Name

Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO aliuliza:- Je, Serikali ina maelezo gani juu ya kero sugu ya kukatika umeme mara kwa mara Handeni Mjini na ni lini kero hiyo itatatuliwa?

Supplementary Question 3

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Iringa hasa Jimbo la Kalenga, kumekuwa na kukatika kwa umeme mara kwa mara na wananchi wanapata adha kwa sababu ya miundombinu chakavu. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha kwamba miundombinu hiyo chakavu inarekebishwa?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa swali zuri la Mheshimiwa Mbunge. Tunayo mikakati kwa ajili ya kuendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika Mkoa wa Iringa. Moja, kuendelea kuboresha miundombinu, kubadilisha nguzo, pamoja na kurekebisha waya chakavu.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, katika Mkoa wa Iringa kwenda Tunduma hadi Katavi tunao mradi mkubwa unaoitwa TAZA wa njia ya kusafirisha umeme ambao unajenga vituo mbalimbali vya kupoza umeme ikiwepo pale Iringa Mjini, Kisada mpaka kufika Mbeya na Tunduma. Vituo ambavyo vitaboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika maeneo yote ya wilaya ya ukanda huu kutoka Iringa, Mbeya, Tunduma mpaka Katavi; na ndio mradi ambao utakwenda kuunganisha gridi yetu pamoja na ya Zambia.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tunafanyia kazi na hali ya upatikanaji wa umeme katika Jimbo la Kalenga na Mkoa wa Iringa itaendelea kuimarika.

Name

Hassan Zidadu Kungu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kaskazini

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO aliuliza:- Je, Serikali ina maelezo gani juu ya kero sugu ya kukatika umeme mara kwa mara Handeni Mjini na ni lini kero hiyo itatatuliwa?

Supplementary Question 4

MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Ninaishukuru na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuwashia umeme katika vijiji vyote kwenye Jimbo la Tunduru Kaskazini, lakini pia na baadhi ya vitongoji vichache katika Jimbo lile. Je, sasa ni lini Serikali itapeleka umeme katika vitongoji vyote vilivyosalia ambavyo havina umeme katika Jimbo la Tunduru Kaskazini?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inao mkakati. Kwa sasa hivi tunayo miradi ya vitongoji ambayo inaendelea katika Jimbo hili la Mheshimiwa Mbunge. Tunayo Miradi ya Ujazilizi (IIC), lakini tuna Mradi wa Vitongoji 15 kwa kila Mbunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa Mradi unaokuja wa Vitongoji 9,000 katika Jimbo la Mheshimiwa Mbunge vitapelekwa vitongoji takribani 54. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inao mkakati wa kuendeleza miradi ya vitongoji katika Jimbo hilo, lakini tutaendelea kuwasimamia wakandarasi ili waweze kutekeleza miradi hii kwa wakati.

Name

Abdallah Jafari Chaurembo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbagala

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO aliuliza:- Je, Serikali ina maelezo gani juu ya kero sugu ya kukatika umeme mara kwa mara Handeni Mjini na ni lini kero hiyo itatatuliwa?

Supplementary Question 5

MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara katika Jimbo la Mbagala, kunakosababishwa na ubadilishwaji wa nguzo kwa muda wa saa 18 kwa siku. Je, zoezi hili kwa nini lisiwe linaishia saa kumi na moja ili wananchi waweze kupata umeme kuanzia saa 12 mpaka alfajiri?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa swali zuri la Mheshimiwa Mbunge. Ni kweli tunafanya marekebisho makubwa kwa ajili ya kuendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme Mbagala. Tumepokea ushauri wa Mheshimiwa Mbunge tutaufanyia ili kuhakikisha kwamba pamoja na kufanya ukarabati wa miundombinu basi tunasaidia vilevile wananchi shughuli zao za kiuchumi na kijamii ziweze kuendelea kwa kupunguza bughudha. Ahsante.

Name

Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO aliuliza:- Je, Serikali ina maelezo gani juu ya kero sugu ya kukatika umeme mara kwa mara Handeni Mjini na ni lini kero hiyo itatatuliwa?

Supplementary Question 6

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi. Mradi huu wa Gridi Imara ambao unaanzia Mkata hadi Kilindi wenye thamani ya shilingi 98,500,000,000 ni mradi muhimu sana kwa sababu dhamira yake ukiacha katikakatika ya umeme, lakini pia ni kwenda katika maeneo ambayo yana migodi na hususan katika Wilaya ya Kilindi ambayo ina migodi mingi. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri uko tayari kuhakikisha kwamba unalisukuma jambo hili ili wawekezaji na wachimbaji wadogo waweze kunufaika na mradi huu? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Mradi huu wa kujenga Kituo cha Kupooza Umeme Kilindi na njia ya kusafirisha umeme kutoka Mkata - Handeni mpaka Kilindi ni mradi muhimu sana kwa ajili ya wananchi wa Kilindi na tulifika pale na Mheshimiwa Rais na aliahidi kwamba mradi huu utaendelea kutekelezeka kwa wakati. Kwa sasa mradi umefikia 30%, mkandarasi yupo site nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Serikali itaendelea kumsimamia mkandarasi ili muda wa kukamilisha mradi ambao ni Aprili, 2026, utakapofika basi mradi huu na wenyewe uwe umekamilika. (Makofi)