Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 6 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 69 2025-04-15

Name

Nashon William Bidyanguze

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Kusini

Primary Question

MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza:-

Je, lini Serikali itapeleka fedha za kujenga majengo katika Kituo cha Afya Kazuramimba - Uvinza?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha afya Kazuramimba katika Halmashauri ya Uvinza kinahudumia wananchi wapatao 40,711.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali imetenga shilingi milioni 625 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wazazi, jengo la upasuaji, jengo la maabara, jengo la kuhifadhi maiti na kichomea taka katika Kituo cha Afya Kazuramimba katika Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza. Ahsante.