Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Nashon William Bidyanguze
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kigoma Kusini
Primary Question
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha za kujenga majengo katika Kituo cha Afya Kazuramimba - Uvinza?
Supplementary Question 1
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, ninaomba kuuliza maswali mawili. Swali la kwanza; Serikali iliahidi hapa Bungeni kupeleka shilingi milioni 50 kwenye Kituo cha Afya pale Nguruka ambacho kimechakaa. Mheshimiwa Waziri Mkuu alishafika pale kuhakikisha. Je, ni lini fedha hizi zitapelekwa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; nina vituo vinne vya Kalya, Buhingu, Ilagala pamoja na Uvinza, vyote miundombinu haijakamilika kwa maana ya wodi pamoja na majengo mengine. Ni lini fedha zitapelekwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hiyo?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Kituo cha Afya cha Nguruka katika Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza ni moja ya vituo vya afya ambavyo vinahitaji kuongezewa majengo na ninafahamu kwamba lilikuwa ni agizo la Mheshimiwa Waziri Mkuu na sisi Ofisi ya Rais, TAMISEMI kama ilivyo ada maelekezo ya Viongozi Wakuu wa Kitaifa ni kipaumbele namba moja. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Bidyanguze kwamba tayari tumeshaliweka kwenye mpango wa fedha za Benki ya Dunia (World Bank) na tunatarajia kupeleka fedha hizo Nguruka mapema iwezekanavyo mwishoni mwa mwaka huu wa fedha au mwanzoni sana mwa mwaka ujao wa fedha 2025/2026.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili kuhusiana na hivyo vituo vya afya vinne ambavyo Mheshimiwa Mbunge amevitaja, ninafahamu ni kweli tuna vituo vya afya ambavyo vina miundombinu pungufu kwa kadiri ya standard ya vituo vya afya na tumeweka mpango tulianza na awamu ya kwanza ya ujenzi tumekamilisha, huduma za msingi zinatolewa. Tutakwenda na awamu ya pili na tutahakikisha pia vituo hivyo tunavipa kipaumbele kwa ajili ya kumalizia majengo hayo yanayohitajika. Ahsante sana.
Name
Prof. Patrick Alois Ndakidemi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Vijijini
Primary Question
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha za kujenga majengo katika Kituo cha Afya Kazuramimba - Uvinza?
Supplementary Question 2
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Wananchi wa Kata ya Kimochi wana hamu kubwa sana ya kupandisha Zahanati ya Shia iwe kituo cha afya. Je, Serikali iko tayari kusaidia wananchi hawa kufikia azma yao hii? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Serikali tuliweka utaratibu kwa kila zahanati ambayo menejimenti ya wilaya inaona kuna sababu ya kuipandisha hadhi kuwa kituo cha afya kuna utaratibu ambao wanatakiwa kuufuata. Kwa hiyo, ninaomba nitumie nafasi hii kumwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kwamba wafanye tathmini kwenye hiyo Zahanati ya Shia kwa maana ya idadi ya wananchi waliopo, lakini pia ukubwa wa eneo na walete maombi ya kupandisha hadhi kuwa kituo cha afya ili Serikali ifanye tathmini na kutenga fedha kwa kushirikiana na halmashauri na Serikali Kuu kwa ajili ya kupandisha hadhi. Ahsante. (Makofi)
MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri wa Fedha.
WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba ku-declare interest, Baba mkwe, juzi nilikuwa pale kwenye msiba na nikushukuru Mheshimiwa Mwenyekiti na Waheshimiwa Wabunge. Mheshimiwa Mbunge pamoja na Mheshimiwa Diwani walilileta jambo hili kwa njia hiyo hiyo. Niseme tu kama alivyojibu Mheshimiwa Naibu Waziri basi Mkurugenzi aharakishe kukamilisha taratibu hizo ili Wizara yetu, Wizara ya TAMISEMI, Mheshimiwa Mbunge pamoja na Diwani wake walivyolileta Serikali iweze kulifanyia kazi. (Makofi)
Name
Anne Kilango Malecela
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Same Mashariki
Primary Question
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha za kujenga majengo katika Kituo cha Afya Kazuramimba - Uvinza?
Supplementary Question 3
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru. Niseme kwamba ninaishukuru sana Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwa kunijengea Kituo cha Afya cha Mtii na Kituo cha Afya cha Myamba, lakini vituo hivi vya afya vyote viwili vimeletewa vitanda vya kulalia wagonjwa, lakini wodi kwa ajili ya kulala wagonjwa bado hazijajengewa. Mheshimiwa Waziri, utawaambia nini hawa wananchi ambao wana hamu ya kuona kwamba wale wanaozidiwa wanalala hospitalini? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niwahakikishie wananchi wa Jimbo la Same Mashariki kwamba Serikali imeshapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo hivyo vya afya vya Mtii na Myamba na tunafahamu kwamba wameshaanza kupata huduma katika vituo vile, lakini tunafahamu kwamba kuna upungufu wa majengo hususan wodi, wodi za wanaume, wanawake na watoto.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niwahakikishie kwamba Serikali imeweka mpango mkakati wa kwenda kujenga majengo hayo katika hivyo vituo viwili, lakini pia katika vituo vingine vyote hapa nchini ambavyo vina upungufu wa miundombinu hiyo tutakwenda kujenga kwa awamu. Ahsante.
Name
Omari Mohamed Kigua
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilindi
Primary Question
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha za kujenga majengo katika Kituo cha Afya Kazuramimba - Uvinza?
Supplementary Question 4
MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa sensa ya mwaka juzi Kata ya Kibirashi ina watu takribani 34,000, lakini wananchi wao hawana kituo cha afya. Je, nini mpango wa Serikali wa kuwajengea kituo cha afya? Ninakushukuru. (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Kibirashi tayari imeshaingizwa kwenye kipaumbele cha vituo vya afya vya kimkakati kwa sababu inakidhi vigezo kwa idadi ya wananchi 34,000 plus. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Kigua kwamba tuko kwenye utaratibu wa kutafuta fedha kwa ajili ya kwenda kujenga kituo hicho cha afya.
Name
Tumaini Bryceson Magessa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Primary Question
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha za kujenga majengo katika Kituo cha Afya Kazuramimba - Uvinza?
Supplementary Question 5
MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini Serikali itaongeza majengo kwenye Kituo cha Afya cha Chikobe ambacho kilijengwa mwaka 1977? Ninakushukuru sana.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ilifanya tathmini na kuorodhesha vituo vya afya vyote vikongwe hapa nchini ambavyo vimejengwa miaka ya 1980 kurudi chini kikiwemo Kituo cha Afya cha Chikobe ambacho kimejengwa mwaka 1974 na Serikali inatambua kwamba miundombinu ile ni chakavu, lakini pia ni pungufu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba tumeshaorodhesha vituo vya afya 215 ambavyo ni vikongwe na chakavu kikiwemo Kituo hicho cha Afya cha Chikobe. Baada ya kukamilisha ukarabati wa hospitali za halmashauri zilizosalia tutatenga fedha na tutakwenda kukarabati na kuongeza miundombinu hiyo. Ahsante sana.
Name
Boniphace Nyangindu Butondo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kishapu
Primary Question
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka fedha za kujenga majengo katika Kituo cha Afya Kazuramimba - Uvinza?
Supplementary Question 6
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kituo cha Afya cha Mwangalanga kina upungufu mkubwa wa majengo ya wodi kwa ajili ya akinamama, watoto na akinababa. Ni lini sasa Serikali itakwenda kujenga majengo hayo muhimu? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaanza utekelezaji wa awamu ya pili wa ujenzi wa miundombinu katika vituo vya afya vyenye majengo pungufu na tutatoa kipaumbele katika kituo hicho cha afya katika Jimbo la Kishapu. Ahsante.