Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 6 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 70 2025-04-15

Name

Mrisho Mashaka Gambo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arusha Mjini

Primary Question

MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza na kumaliza ujenzi wa stendi ya kisasa ya Jiji la Arusha katika eneo la Bondeni City?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Jiji la Arusha ni miongoni mwa Miji 45 wanufaika wa Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Miji ya Tanzania (TACTIC). Jiji hili lipo katika kundi la kwanza ya utekelezaji yenye Miji 12 ambapo tayari miradi ya awamu ya kwanza ya barabara na mitaro yenye thamani ya takriban shilingi bilioni 20 ilianza kutekelezwa kwa kusaini mikataba ya Ujenzi Septemba, 2023.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kukosekana kwa wakandarasi wenye vigezo kupitia zabuni zilizotangazwa Machi, 2024, katika miji minne ikiwemo Halmashauri ya Jiji la Arusha, Serikali imetangaza zabuni ya kumpata mkandarasi kwa mara ya pili (Re-advertisement) tarehe 11 Machi, 2025. Mchakato huu unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Aprili, 2025 ambapo mshindi atatangazwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji unatarajiwa kuanza mwezi Mei, 2025 ambapo ujenzi huu unatarajiwa kuwa wa mwaka mmoja na unatarajiwa kukamilika ifikapo Mei, 2026. Ahsante.