Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mrisho Mashaka Gambo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arusha Mjini
Primary Question
MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza na kumaliza ujenzi wa stendi ya kisasa ya Jiji la Arusha katika eneo la Bondeni City?
Supplementary Question 1
MHE. MRISHO M. GAMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafahamu kwamba Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ametutafutia Mradi wa TACTIC kwa ajili ya kujenga stendi hii na fedha zipo. Sasa nina maswali yangu mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza; tumekuwa tukipata majibu ya Serikali ndani ya Bunge hili ambayo hayatekelezeki zaidi ya mara nne. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yupo tayari kujiuzulu endapo ikifika Mwezi Mei mwaka huu mkandarasi hajakwenda site kule Bondeni City kwa ajili ya kuanza ujenzi wa stendi ya kisasa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kumekuwa na baadhi ya viongozi wamekuwa wanatoa kauli ya kwamba mchakato wa ujenzi wa stendi umekwama kwa sababu ya Mbunge. Je, Serikali iko tayari kutoa majibu kwa wananchi wa Jimbo la Arusha Mjini, ni nini hasa kinakwamisha kuanza kwa ujenzi wa stendi?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kumhakikishia Mheshimiwa Mrisho Mashaka Gambo, Mbunge wa Arusha Mjini, kwamba tunafahamu ni kweli Serikali imekuwa na dhamira ya dhati kama ilivyo dhamira ya Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kutenga mabilioni ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa stendi na miundombinu mbalimbali katika Jiji la Arusha. Ni kweli kwamba baadhi ya miundombinu kazi imeanza, lakini tunafahamu sana umuhimu wa stendi ya Bondeni City katika Jiji la Arusha, ila lazima taratibu za manunuzi zifuatwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ilitangaza zabuni, wazabuni walipatikana, lakini hawakukidhi vigezo kwa mujibu wa Sheria na Taratibu za Manunuzi na Serikali isingeweza kuendelea kumpa mkandarasi ambaye hajakidhi vigezo, ingekuwa ni ukiukaji wa sheria. Kwa hiyo, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba dhamira ya Serikali ni thabiti iko palepale na sasa tuko hatua za mwisho za kumpata mkandarasi na tunaamini ifikapo mwezi Mei mwaka huu ujenzi utaanza na utakamilika ndani ya wakati ifikapo mwezi Mei, 2026.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, si kweli kwamba Mheshimiwa Mbunge wa Arusha Mjini ndiye anayekwamisha ujenzi wa Stendi ya Bondeni City. Si kweli kwa sababu taratibu za manunuzi zimekuwa zikiendelea na kumekuwa na upungufu kwa wakandarasi waliopatikana na Serikali imeendelea kuhakikisha kwamba inafanya re-advertisement ili mkandarasi sahihi kwa mujibu wa sheria apatikane. Kwa hiyo, ninaomba niwahakikishie wananchi wa Jiji la Arusha kwamba Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo hilo amekuwa akifuatilia mara kwa mara na Serikali hii sikivu ya Awamu ya Sita itahakikisha inatekeleza mradi huo kwa wakati. (Makofi)
Name
Suma Ikenda Fyandomo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza na kumaliza ujenzi wa stendi ya kisasa ya Jiji la Arusha katika eneo la Bondeni City?
Supplementary Question 2
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Mkoa wa Mbeya ni Jiji, lakini hauna stendi yenye hadhi ya jiji. Niliuliza swali hili na wananchi wa Mkoa wa Mbeya wamenituma niulize tena kwa sababu majibu yale hawayakuelewa vizuri. Je, ni lini Serikali itajenga stendi ambayo ina hadhi ya Jiji la Mbeya? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli na ni muhimu sana Jiji la Mbeya kuwa na stendi ya kisasa inayofanana na hadhi ya jiji na Serikali hii imeweka kipaumbele na imeweka mipango ya kwenda kutekeleza ujenzi wa stendi ya kisasa katika Jiji la Mbeya. Ninafahamu kwamba Jiji la Meya ni moja ya majiji ambayo yako kwenye mpango wa TACTIC na ninafahamu katika package ya TACTIC tutahakikisha pia tunaweka utaratibu wa kuanza ujenzi wa stendi hiyo mapema iwezekanavyo na kwa wakati ili Jiji la Mbeya na wananchi wake wapate huduma bora za usafiri. Ahsante.
Name
Fatma Hassan Toufiq
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza na kumaliza ujenzi wa stendi ya kisasa ya Jiji la Arusha katika eneo la Bondeni City?
Supplementary Question 3
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza. Je, lini Serikali itajenga stendi ya kisasa katika Jiji la Dodoma hasa kwa ajili ya daladala kwani eneo la Nyerere Square limekuwa na msongamano mkubwa sana na kuleta karaha kwenye nchi? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie tu Mama yangu Mheshimiwa Toufiq kwamba Serikali hii moja ya kipaumbele kilichowekwa kwenye miundombinu ya usafiri ni kujenga stendi za kisasa za mabasi lakini pia stendi za kisasa za magari madogomadogo kwa maana ya daladala. Jiji la Dodoma ni Makao Makuu ya nchi na ni Jiji linalokua kwa kasi, nimhakikishie tu kwamba, tayari mipango imeshawekwa kwa ajili ya kwenda kujenga stendi hizo kwa awamu. Kwa hiyo, tutakwenda kujenga stendi hiyo ili usafiri huo pia uwe katika mazingira bora zaidi. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved