Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 6 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 71 2025-04-15

Name

Neema Gerald Mwandabila

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA G. MWANDABILA aliuliza:-

Je, Serikali imefikia hatua gani katika kuhakikisha fursa zote za mikopo zinatolewa kwa uwiano unaozingatia usawa katika halmashauri zote?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imesanifu mfumo wa kidijiti wa WEZESHA Portal, Mfumo wa Kugawa Mapato ya 10% ya Halmashauri kwa Makundi Maalumu ili kuhakikisha kuwa taarifa za mikopo zinachakatwa na kusimamiwa kwa uwazi na kwa usawa ili kuondoa dosari mbalimbali wakati wa utoaji wa mikopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Serikali imeweka utaratibu ambao maombi yote ya mikopo hujadiliwa katika Kamati ya Huduma ya Mikopo ngazi ya kata; Kamati hiyo ngazi ya halmashauri na Kamati hiyo ngazi ya wilaya kufanya uhakiki wa mikopo, lakini timu ya menejimenti, Kamati ya Kudumu ya Fedha, Uongozi na Mipango na Kamati ya Kudumu ya Fedha na Utawala; Baraza la Madiwani; Kamati ya Bajeti ya Halmashauri; na mwisho Kamati ya Uratibu wa Mikopo ngazi ya mkoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa utaratibu uliofanywa na kuidhinishwa na Serikali unatoa fursa kwa mikopo inayotolewa na Halmashauri kwa wajasiriamali wa makundi maalum kuwa na usawa na kuwezesha kufanya shughuli za kiuchumi na kujiongezea kipato. Ahsante.