Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 6 | Planning and Investment | Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji). | 72 | 2025-04-15 |
Name
Taska Restituta Mbogo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:-
Je, lini Serikali itawalipa wastaafu waliokuwa wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyovunjwa mwaka 1977?
Name
Prof. Kitila Alexander Mkumbo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ubungo
Answer
WAZIRI WA FEDHA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Mipango na Uwekezaji, ninaomba kujibu swali kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, waliokuwa wafanyakazi wa lililokuwa Shirika la Posta na Simu Tanzania (Tanzania Posts and Telecoms Corporation) pamoja na Shirika la Reli la iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, walilipwa mafao yao ya mkupuo kupitia Ofisi ya Mlipaji Mkuu wa Serikali mwaka 2005. Hata hivyo, baada ya malipo hayo, baadhi yao walirudi kudai mapunjo ambapo Wizara iliyafanyia kazi kulingana na taratibu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2009 Serikali iliwarejesha wastaafu hao kwenye daftari la pensheni ambapo wanalipwa kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina. Wastaafu hao kwa sasa wanalipwa pensheni yao ya kila mwezi kwa utaratibu wa miezi mitatu, mitatu. Aidha, hadi sasa Serikali imelipa pensheni ya kipindi cha Aprili, 2025 hadi Juni, 2025 kiasi cha shilingi bilioni 1,085 kwa wafanyakazi 1,794 kama ambavyo imetengwa na yaliyokuwa mashirika ya EAC, TTCL, TRC, TPC pamoja na TPA.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved