Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Taska Restituta Mbogo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:- Je, lini Serikali itawalipa wastaafu waliokuwa wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyovunjwa mwaka 1977?

Supplementary Question 1

MHE. TASKA R. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; Jumuiya ya Afrika Mashariki ilikuwa na taasisi mbalimbali ambazo zilikuwa ni Telecommunication, Cargo Handling, Railway, Airways na Harbors, lakini majibu ya Serikali ni kwa taasisi mbili. Je, Serikali iko tayari kukaa na taasisi nyingine ambazo zilikuwa kwenye East African Community ili kuangalia madai yao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa waliokuwa wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyovunjika mwaka 1977, wanadai kwamba Serikali iliwalipa pesa zao pungufu na kwamba Serikali haikufuata tathmini iliyotolewa na liquidator. Je, Serikali iko tayari kuunda tume na kukaa na wafanyakazi hawa ili kupata muafaka na waweze kulipwa pesa zao? (Makofi)

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA FEDHA K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia masuala haya ya wazee wetu. Niseme kwamba kwa niaba ya Serikali tunapokea wazo lake kwamba kuna baadhi ya taasisi nyingine ambazo bado wanahitaji kukaa na Serikali na Serikali imekuwa ikifanya hivyo na hivyo ndivyo ilivyovifikia hatua hii kwenye hizi taasisi nilizozitaja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu wale wengine ambao wameongelea kama alivyotoa hoja ya mapunjo pamoja na taratibu alizozisema ili ziweze kufuatwa kikamilifu, tumelichukua. Pia, utaratibu wa Serikali wa kulipa madai na madeni punde yanapojitokeza kama hivi ambavyo Mheshimiwa Mbunge amesema, huwa yanafanyiwa uhakiki na hoja hizo zinaangaliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, zinaangaliwa na Ofisi ya Attorney General, zinaangaliwa na Mkaguzi wa Ndani pamoja na idara nyingine zinazoshughulikia masuala ya aina hiyo. Kwa hiyo, tumelipokea, lakini Serikali itafanyia kazi maeneo hayo yote mawili.