Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 6 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 73 2025-04-15

Name

Abdi Hija Mkasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Micheweni

Primary Question

MHE. ABDI HIJA MKASHA aliuliza:-

Je, Kamera zilizofungwa Mji Mkongwe Zanzibar zinasaidiaje katika kupambana na kudhibiti uhalifu kwenye maeneo haya?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mji Mkongwe Zanzibar zimewekwa kamera na zilianza kufanya kazi kuanzia tarehe 3 Oktoba, 2018. Matumizi na usimamizi wake unaratibiwa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Lengo la kuwekwa kamera ni kudhibiti uhalifu na kufuatilia matukio ya kihalifu yanayotendeka. Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2018 hadi 2025 kamera hizo zimesaidia kutambua, kufuatilia na kukamatwa matukio 1,177 ya uhalifu. Uwepo wa kamera hizo, umesaidia sana kudhibiti uhalifu na matukio ya kihalifu katika maeneo ya mji Mkongwe. Ahsante.